Habari

Mahakama yaamuru msichana aliyevuliwa nguo na polisi alipwe milioni 90

Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru Serikali kumlipa Mwanafunzi wa kike tsh milioni 9o baada wa kuvuliwa nguo na polisi waliokuwa wakitafuta madawa ya kulevya katika shule ya Sekondari ya Kanyama mjini  Karatina mnamo mwaka 2015.

Picha za msichana huyo mwenye miaka 18 zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuchukuliwa na polisi hao ambao walikuwa wanafanya msako wa kukagua madawa ya kulevya aina ya bangi.

Kwa mujibu wa Gazeti la Standard limeripoti kuwa msichana huyo alipopigwa picha akiwa nusu uchi na kisha picha zake kusambazwa aliamua kwenda mahakamani kulishtaki jeshi la polisi.

Msichana huyo ambaye alisaidiwa na Shirika la kupigania haki za watoto la (CRADLE Children’s Foundation) alipeleka kesi hiyo mahakamani wakidai kuwa picha hizo zilimuathiri na kutaka alipwe milioni 7 za Kenya.

Gazeti la Standard lilisema kuwa msichana huyo alikuwa miongoni mwa wanafunzi wengine 44 waliokamatwa katika kituo cha biashara cha Kibirigwi trading centre katika Kaunti ya Nyeri wakiwa kwenye gari wakivuta bangi na kufanya mapenzi wakati wakirejea nyumbani kipindi cha likizo.

Chanzo : Gazeti la Standard 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents