Habari

Maisha yatakuwa bora kwako ukiacha haya

Maisha hayabadiliki mpaka utakapoamua kubadilisha mfumo wako mwenyewe. Utakapoacha kuona changamoto ni vizuizi vya kutofanya vitu. Utakapoacha kuona mtaji ni kikwazo cha wewe kutofanya biashara.

header_initiative_lifestyle_bg

Utakapoacha kuona usiku ni muda wa kulala na kugundua usiku ni muda mzuri sana wa kufanya kazi ya ziada kwa utulivu zaidi. Utakapo acha visingizio za kuanza kwa sababu unafikiri hujajipanga. Utakapoacha kuamini watu wanasemaje kuhusu wewe na wewe unawaza nini kuhusu wao?

Utakapoacha kutegemea mshahara na kuanza kufanya vitu vitakavyokupa kipato cha ziada na mshahara ubakie kuwa ziada ya  yakufanyia manunuzi ya matumizi mengine lakini si kisababishi cha maisha. 

Utakapoacha kuamini kwamba lazima uajiriwe ili uweze kuishi na kwamba bila ajira utakufa njaa. Utakapoacha kuangalia waliofeli kama sababu ya wewe kutokufanya walichofanya kwa hofu kwamba walifeli na wewe utafeli.

Utakapoacha kuamini kwamba ukimaliza shule lazima uajiriwe ili utoke kimaisha na kuanza kuwaza jinsi stashahada/shahada yako uliyopata ikusaidie vipi kuandaa kitu chako?  Utakapoacha kuogopa kukutana  na watu wakubwa na waliokuzidi kwa kuona kuwa unajishusha na kujichoresha sababu hata ukijifanya hutaki kuchoreka ndo unajichoresha kwasababu utabaki na maisha hayo hayo na wao kuendelea kuwa juu maisha yao yote na gepu litakuwa kubwa zaidi. Watabaki wanajua na wewe hujui na unaficha kutokujua kwako. Ni heri ujishushe ili ujifunze waliwezaje ili na wewe uweze kuwa kama wao au zaidi ya pale walipofika.

Maisha hayana miujiza ukitaka maisha yabadilike badilisha yote unayofanya sasa kwa kawaida na ufanya zaidi na utaona utofauti mkubwa.

Usitegemee mabadiliko kwenye maisha yako kama unaendeleea kufanya mambo yale yale katika maisha yako. Mungu sio Kalumanzila ametupa vyote tuvitumie kwa akili. Ukifeli sio kosa la Mungu, unawajibika asilimia 100 kwa kushindwa kwako kwenye maisha. Mungu alishaumba dunia na vyote,kushindwa kwako kutumia sio kosa lake. Badilika leo kimtazamo ubadilishe maisha yako.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents