Tupo Nawe

Manusura ajali ya Ndege Pakistan asimulia ilivyokuwa, “Nilichokiona ni moto tu”

Mmoja wa watu walionusurika ajali ya ndege siku ya Ijumaa nchini Pakistani katika mji wa Karachi aelezea kuhusu tukio hilo ambalo analiona kama ndoto ya kutisha, anasema alikuwa anaona moto tu.

Abiria wa ndege ya Pakistan Muhammad Zubair ni miongoni mwa abiria wawili ambao walinusurika katika ajali hiyo ya ndege ya kimataifa ya ‘Pakistan International Airlines (PIA) Airbus A320’ iliyoanguka katika makazi ya watu.

Mamlaka ya afya katika jimbo la Sindh imesema kuwa vifo 97 vimethibitishwa .

Chanzo cha ajali kikiwa hakijafahamika bado.

Rubani aliripoti tatizo la kiufundi baada ya jaribio la kwanza la kutua kushindwa, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo kisha akapiga simu wakati ndege inaanguka.

Ajali hii imetokea siku chache tu baada ya mamlaka ya Pakistan kuruhusu ndege za biashara kuanza shughuli zake baada ya kulegeza masharti kutokana na hatua ya kutotoka nje kuzuia maambukizi ya corona.

Muhammad Zubair aliwezaje kupona ajali hiyo?

Ndege namba PK8303, Airbus A320 ambayo ilikuwa na abiria 91 na wafanyakazi wanane wa ndege hiyo – ilikuwa na familia nyingi ambazo zilikuwa zinasafiri kwa ajili ya mapumziko ya sherehe za Eid siku ya Jumapili – walikuwa wanasafiri kutoka Lahore.

Ndege hiyo ilikuwa inajaribu kutua uwanja wa kimataifa wa Jinnah uliopo mjini Karachi majira ya saa nane na nusu saa za taifa hilo wakati ilipoanguka.

Bwana Zubair, ambaye alipata majeraha kidogo anasema ndege ilikuwa inataka kushuka katika uwanja wa ndege lakini ikashindwa na kupata ajali dakika 10-15 baadae.

“Hakuna ambaye alifahamu kuwa ndege ilikuwa inaenda kuanguka, safari ilikuwa nzuri tu na hatukuhisi utofauti wowote,” alisema.

Nilipoteza fahamu baada ya ajali, “Wakati ambao nimezinduka nilisikia tu kelele za watoto na watu wazima kila kona. Nilichokiona ni moto tu. Nilikuwa sioni mtu yeyote zaidi ya kelele nyingi za vilio “.

” Nilifungua mkanda wa kiti changu na kuona mwanga – nikaanza kufuata mwanga na ilinibidi niruke kama mita 3 (futi 10) ili kuwa salama”, aliongeza.

Map of Pakistan highlighting Lahore and Karachi
Presentational white space

Ajali iliyokea eneo la makazi

Kwa nini ndege hiyo ilianguka?

Ndege ilikuwa karibu na usawa wa makazi ya watu wakati ilipogonga majengo yaliyojengwa wakati wa ukoloni.

Picha za video zinaonyesha jinsi kikosi cha uokoaji kilivyokuwa kinajaribu kuokoa watu waliokuwa katika eneo hilo.

Magari kadhaa yalishika moto pia.

Shahidi wa tukio hilo Mohammed Uzair Khan ameliambia shirika la BBC kuwa alisikia sauti za watu wengi nje ya nyumba yake.

“Karibu nyumba nne ziliharibiwa kabisa, kulikuwa na moto mkubwa na moshi mwingi,” alisema. “Walikuwa majirani zangu, siwezi kuelezea tukio lilikuwa baya kiasi gani?”

Mawasiliano kati ya mwongozaji ndege na rubani yalichapishwa katika vyombo vya habari vya Pakistani. Rubani alisikika akisema ndege ilikuwa inahitilafu katika ‘injini”.

Mwongozaji wa ndege alikuwa anamuuliza rubani kama anaweza kuendelea kuishusha ndege hiyo”, na rubani alikuwa anajibu kwa ishara kuwa bado kuna shida.

Maofisa wa masuala ya anga wameiambia Reuters kuwa ndege hiyo ilishindwa kufuata uelekeo wake.

Picha ziliwekwa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha kuwa ndege ilikuwa inatatizo kwenye injini zake zote na isingeweza kufika katika eneo ambalo lilikusudiwa.

Wachunguzi watajaribu kuona nini ambacho kipo katika kisanduku cha sauti cha kwenye ndege ‘black box’ ili waweze kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Kamati ya uchunguzi wa ajali hiyo tayari imepangwa.

Ndege hiyo ambayo ilianza kufanya kazi mwaka 2014 na ilifanyiwa ukaguzi mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana.

rescue workers search the wreckageHaki miliki ya pichaAFP
Image captionNdege ilianguka katika makazi ya watu

Tunafahamu nini kuhusu watu waliofariki katika ajali hiyo?

Kwa mujibu wa mamlaka ya nchi hiyo, vifo 97 vimethibitishwa ingawa haijawekwa wazi katika idadi hiyo wangapi ni abiria wa ndege na wangapi ni wakazi wa eneo hilo.

Maiti 19 ziliweza kufahamika.

Rais wa benki ya Punjab, Zafar Masud, ni miongoni mwa watu walionusurika katika ajali hiyo, alisema msemaji wa serikali.

Mwandishi wa habari wa chaneli ya TV ya 24 News, Ansar Naqvi, na aliyekuwa meneja wa mamlaka wa majanga wa Punjab, Khalid Sherdil, walikuwa katika orodha hiyo ya abiria ambao labda wamenusurika.

relative of one of the victims mournsHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWengi waliokuwa wanassafiri ni familia zilizokuwa zinaenda kusherehekea sikukuu ya Eid

Jumamosi ibada ya mwisho kwa baadhi ya waathirika ilifanyikamjini Karachi. Vipimo vya vinasaba vinafanyika kubaini miili ya wengine kabla ya kukabidhiwa familia zao.

Waziri mkuu wa Pakistan, Imran Khan alisema alishtuka na kusikitishw ana ajali hiyo na kuahidi kufanyika kwa uchunguzi haraka iwezekanavyo.

Lakini Chama cha Shirika la Ndege la Pakistan kimesema hakina imani na uchunguzi huo na kimeita wachunguzi wa kimataifa kujuika katika jopo la uchunguzi wa ajali.

Rekodi ya usalama wa anga Pakistan inasema?

Licha ya kwamba mamlaka ya anga inajisifu katika utendaji wake, lakini historia ya ajali za ndege iko hivi nchini Pakistani;

Mwaka 2010,ndege binafsi ya Airblue ilipata ajali karibu na Islamabad, na kuua watu wote kwenye ndege ambao walikuwa 152 – hii ni ajali mbali Zaidi kutokea nchini Pakistan.

Mwaka 2012, ndege aina ya Boeing 737-200 ambayo ilikuwa inafanya safari zake Pakistan- Bhoja Air ilipata ajali mbaya ikiwa inakaribia kutua Rawalpindi,na kuuwa abiria wote 121 na wahudumu wa ndege sita.

Na mwaka 2016, ndege ya kimataifa ya Pakistan ililipuka wakati ilikiwa inaelekea magharibi mwa Pakistan kuelekea Islamabad, na kuua watu 47.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW