Burudani

Mariah Carey asherehekea miaka 20 ya ‘Butterfly’

Msanii wa muziki kutoka nchini Marekani, Mariah Carey amesherehekea miaka 20 ya uwepo wa albamu yake ya’Butterfly.

Albamu hiyo iliyotoka mwaka 1997, chini ya lebo ya Columbia Records iliyokuwa ikisimamiwa na mumewe wa kwanza Tommy Mottola, iliuza zaidi ya kopi milioni 50 ndani ya miaka mitano.

Akiongea katika kipindi cha VH1, Mariah amewashukuru wakongwe wa muziki kama Jermaine Dupri na Combs, walivyoweza kumsaidia katika utayarishaji wa  albamu hiyo.

“People were a little more apprehensive about me doing tracks that had a harder edge or working with people that might not be the typical pop producer,” amesema Mariah.

Kutokana na uwekezaji mkubwa wa fedha katika albamu ya ‘Butterfly’, Mariah  Carey alifikiria kuanzisha  lebo yake ya muziki kutokana na mauzo aliyoyapata.

Kwa sasa msanii huyo msanii huyo anamilki lebo yake inayoyofahamika kama ‘Butterfly MC’.

“I can’t believe #Butterfly is turning 20 today. I wasn’t even born then! My fans and I know that this is “our album”. I’m so happy to celebrate this anniversary with you. ❤? #Lambs, what’s your favorite lyric from the album?#ButterflyAnniversary,” ameandia mrembo huyo katika mtandao wa Instagram.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents