Habari

Masanja Mkandamizaji afiwa na mdogo wake!


Mchekeshaji maarufu wa kundi la Original Comedy Emmanuel Mgaya aka Masanja Mkandamizaji jana amefiwa na mdogo wake.
Kupitia Facebook aliandika, “ndugu nimefiwa na mdogo wangu. Tunaaga Amana kesho halafu tunaelekea kijijini kuzika. Mniweke katika maombi yenu.”
Mdogo wake aitwaye Valle Mgaya alifariki nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam na taarifa zinadai kuwa marehemu alikutwa na mauti hayo akiwa nyumbani kwake.
Mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika Hospitali ya Amana.

Bongo5 inampa pole Masanja kwa msiba huo na Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents