Habari

Mastaa waungana kuiombea Houston baada ya kukumbwa na mafuriko

Mastaa kadha kutoka Marekani, wameamua kuungana na kutaka kuchangia waathirika wa mafuriko yaliyoikumba jimbo la Houston Marekani.

Mafuriko hayo yamesababishwa na kimbunga cha Harvey, kijichotokea katika jimbo hilo na katika maeneo mengine ya mji. Mpaka sasa imeripotiwa kuwa watu 2,000 wameokolewa kutoka na kimbunga hicho na wawili wamesadikika kufa maji.

Mastaa kama Kervin Hart, 50 Cent, Nick Minaj wameamua kuunga mkono kampeni iliyoanzishwa ya kuombea mji huo na kutoa msaada kwa waathirika wa tukio hilo.

Idara ya Taifa ya Hali ya Hewa (NWS) imesema hali ambayo inashuhudiwa katika maeneo mbalimbali katika jimbo hilo haijawahi kutokea, pia idara hiyo imesema kuwa mafuriko yaliyotokea katikati mwa mji huo bado wanendelea na uchunguzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents