Michezo

Maurizio Sarri amkingia kifua Kepa,Tulishindwa kuelewana tu ila hakuna tatizo lolote la kinidhamu” (+ Video)

Katika mchezo uliofanyika usiku wa jana wa fainali za Carabao Cup katika uwanja wa Wembley ambao uliwakutanisha Chelsea na Manchester City na City kufanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara nyingini. lakini tukio lililowashangaza wengi ni lile la Mchezaji kukataa kutoka uwanjani – na meneja wake apoteza muelekeo wa mechi. Kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga alikataa jitihada za meneja Maurizio Sarri kumbadilisha uwanjani katika dakika za ziada za mechi ya fainali ya kombe la Carabao, hatua iliomuacha meneja huyo akiwa na hasira kubwa nje ya uwanja huo.

Arrizabalaga alikuwa amehudumiwa kwa kubanwa kwa maumivu ya msuli, na wakati mechi ikiwa 0-0, Sarri alikuwa anajitayarisha kumuingiza kipa wa akiba Willy Caballero katika nafasi ya Kepa kabla ya awamu ya mikwaju ya penalti.

Lakini baada ya kunyosheana vidole kwa muda kadhaa na kupiga kelele, HAPANA!, ilibidi Sarri asalimu amri.

Refa Jonathan Moss alikimbia kumfuata Sarri kuthibitisha iwapo kweli anataka Arrizabalaga aondoke au la, na Sarri, ilibidi abadili msimamo wake kabla ya kuondoka kwa hasira , na muda mfupi baadaye kurudi, akimuacha kipa wa akiba Caballero akiwa amechanganyikiwa.

Arrizabalaga alifanikiwa kuokoa mkwaju wa Leroy Sane – lakini Raheem Sterling alifunga bao la ushindi katika mikwaju hiyo ya penalti wakati Manchester City walipotuzwa mabingwa wa taji hilo la Carabaokwamwaka wa pili kutokana na ushindi wa mwisho wa mabao 4-3.

Sarri hakuonekana kuonyesha hisia zozote, wakati wachezaji wake wakionekena kuhuzunishwa kwa kushindwa.

Kwa mujibu wa BBC, Aliyekuwa mshambuliaji huko Stamford Bridge Chris Sutton ameeleza matukio ya jana kama ”hujuma kwa Chelsea” na kuapa kwamba Arrizabalaga “hastahili kucheza tena katika klabu hiyo”.

Hilo linajiri kufuatia wiki kadhaa za uvumi kuhusu nafasi ya Sarri kama meneja wa klabu hiyo na wasiwasi kuhusu mbinu zakezilizopewa jina maarufu “sarri-ball”.

“Kama ningekuwa Sarri ningeondoka. Huwezi kudharauliwa. Ni kwanini wachezaji hawakumburura Kepa nje?

“Kepa anastahili kufutwa kazi, sio Sarri. Amedhauriliwa – sio jambo zuri kwa meneja.”

Aliyekuwa mchezaji wa England na timu ya Tottenham Jermaine Jenas anasema ni wazi “hakuna heshima” kwa meneja, lakini amesema Sarri ameonyesha “hana ustaarabu” kwa kuamua kuondoka uwanjani baada ya kushindwa.

Kocha huyo baada ya mchezo alisema:-

“Tulishindwa kuelewana mara baada ya daktari kusema ameumia. Lakini Kepa alikuwa sahihi kusema kuwa yupo sawa kuendelea na mechi.”
“Hakuna tatizo lolote la kinidhamu ila nitamtafuta na kumwelekeza namna ya kuwa mtiifu kila ninapofanya maamuzi” Sarri

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents