Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Mbunge mwingine wa CHADEMA ahamia CCM, Polepole atangaza OFA kwa Wabunge wanaotaka kuhamia CCM

Mbunge wa Simanjiro kwa tiketi ya CHADEMA, James Ole Millya amejiuzulu nafasi ya Ubunge na nafasi zake zote kwenye chama hicho na  kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Image result for James Ole Millya na mbowe
James Ole Millya

Kikubwa zaidi kilichomfanya ahamie CCM ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Maamuzi hayo ameyafanya mchana wa leo, wakati ambao Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM, Humphrey Polepole akitoa tangazo kuwa kwa wabunge na madiwani wa vyama vya upinzani wanaotaka kuhamia CCM mwisho ni mwaka huu 2018.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW