Burudani

MC Pilipili yupo chini ya uangalizi- Dk. Cloud

Hali ya mchekeshaji Emmanuel Mathias maarufu kama MC Pilipili inazidi kutengemaa baada ya kupata ajali siku ya Jumanne akiwa Mkoani Shinyanga.

Kauli hiyo imetolewa na Daktari wa Hospitali ya Bugando, Dk. Cloud asema Emmanuel Mathias (MC Pilipili) yupo chini ya uangalizi na anaendelea vizuri na matibabu.

Awali hapo zilitoka habari kuwa mchekeshaji huyo yupo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu akisubiria kufanyiwa vipimo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alithibitisha kutokea ajali hiyo ambapo alieleza kuwa Mc Pilipili alikuwa akimkwepa mwendesha baiskeli katika Kijiji cha Bubiki, Kata ya Mondo mkoani humo.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents