Tupo Nawe

MEXICO: Meya aburuzwa nyuma ya gari na wananchi kisa kutotimiza ahadi

MEXICO: Meya aburuzwa nyuma ya gari na wananchi kisa kutotimiza ahadi

Watu 11 wamekamatwa na kutiwa mbaroni kwa kosa la kumkamata meya wa kijiji chao kisha kumfunga katika gari na kumburuza mitaa mbalimbali. Polisi waliingia kati tukio hilo kwa na kumuondoa meya Jorge Luis Escandón Hernández ambae alipatwa na majeraha kidogo.

Hili ni shambulio la pili kutoka kwa wakulima hao ambao wanadai hawajatimiziwa ahadi alizotoa meya Hernández, ikiwemo ujenzi wa barabara.

Polisi zaidi wamepelekwa katika kijiji cha jimbo la Chiapas.

hh

Meya pamoja na viongozi wa chini wa serikali mara nyingi hushambuliwa nchini mexico na makundi ya kihalifu wasipofanya matakwa wanayoyataka, lakini kupigwa kwa ahadi za uchaguzi ni jambo geni.

Meya Hernández amesema atafungua kesi ya kutekwa na kutaka kuuwawa.

Video zilizochukuliwa na wapita njia nje ya ofisi ya meya huyo zimeonesha kundi la wanaume wakimvuta nje ya jengo na kumfunga nyuma ya gari.

Picha zilizochukulia na CCTV kamera zinaonesha akiburuzwa huku akiwa amefungwa kamba katika mikono yake katika mitaa ya Santa Rita.

Iliwachukua kundi la polisi kadhaa kuweza kumuokoa katika kadhia hiyo, watu kadhaa walijeruhiwa baina ya polisi na watu hao.

Katika tukio la miezi kadhaa iliyopita watu wasiojulikana walivamia na kuharibu ofisi yake, lakini yeye hakuwepo.

meya

View this post on Instagram

HABARI: WANANCHI WENYE HASIRA KALI WAMBURUZA BARABARANI MEYA WAO, WADAI AMESHINDWA KUTIMIZA AHADI ZAKE Wakazi wa Manispaa ya Las Margaritas, nchini Mexico wamemburuza Meya wa manispaa hiyo, Jorge Luis Escandón Hernández, barabarani wakiwa wamemfunga kwenye gari, Kwa madai kuwa hajatimiza ahadi ya kujenga barabara aliyotoa wakati wa kampeni. Wananchi hao ambao asilimia kubwa ni wakulima kutoka katika eneo la Chiapas, Walimteka Kwanza kiongozi huyo akiwa ofisini kwake na kisha usiku wa manane kumburuza barabarani kama adhabu ya kutotimiza ahadi zake za kampeni. Tayari watu 11 wamekamatwa na kutiwa mbaroni kwa kosa la kumteka kiongozi wao kisha kumfunga katika gari na kumburuza mitaa mbalimbali. Polisi waliingia kati tukio hilo kwa na kumuondoa meya Jorge Luis Escandón Hernández ambae alipatwa na majeraha kidogo. Hili ni shambulio la pili kutoka kwa wakulima hao ambao wanadai hawajatimiziwa ahadi alizotoa meya Hernández, ikiwemo ujenzi wa barabara. Polisi zaidi wamepelekwa katika kijiji cha jimbo hilo, Meya pamoja na viongozi wa chini wa serikali mara nyingi hushambuliwa nchini mexico na makundi ya kihalifu wasipofanya matakwa wanayoyataka, lakini kupigwa kwa ahadi za uchaguzi ni jambo geni. Kwenye uchaguzi Mwaka jana, Meya huyo aliahidi kujenga kwa kiwango cha lami barabara zote zinazoingia mashambani ili kusaidia usafirishaji wa mazao, Lakini mpaka sasa ni mwaka mmoja umepita hajafanya hivyo. Meya huyo ambaye kwa sasa yupo Hospitalini, Mwanasheria wake amesema atawafungulia wananchi mashtaka ya utekaji na jaribio la kuua. WRITTEN BY @mgallahtz .

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

Wakati wa uchaguzi wa kiti cha meya, Hernández alihusishwa pia na ghasia dhidi ya mpinzani wake lakini alichiwa kutoka na kukosekana kwa ushahidi.

Chanzo BBC.
By ALLY JUMA.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW