Burudani

Migos watangaza ujio wa ‘Culture II’

Kundi la Rap linalofanya vizuri kwa sasa Migos, kutoka Marekani wanatarajia kuachia albamu yao ya Culture II ifikapo Januari 26 mwaka huu.

Migos linaloundwa na vijana watatu ambao ni Quavo, Takeoff, na Offset waliachia album ya Culture I Januari 27 mwaka uliopita. Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter wamepost kava ya albamu hiyo na kuandika “C U L T U R E I I ”

Curture II inatarajiwa kuna na ngoma kadhaa ikiwemo ‘MotorSport’ inayofanya vizuri katika chat zambalimbali za muziki ikiwemo Billbords Hot 100 ambapo inashika namba 8, huku ngoma ya ‘Stir Fry ‘ waliofanya na Pharrel inatarajiwa kuwepo.

Albamu ya Culture I,  ilikuwa albamu ya kipekee kwani iliweza kufika namba moja kupitia chat za Billboard 200, kwa muda wa wiki moja  tokea kuachiwa kwake Januari 27, 2017  na ilifanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha tuzo za Grammy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents