DStv Inogilee!

Mimi kama Bi. Kidude, tusipangiane mavazi ya kuvaa – Queen Darleen

Msanii wa muziki nchini Tanzania, Queen Darleen amefunguka kuwa yeye kwenye muziki wake hajawahi kushuka kwenye muziki kama watu wengi wanavyodai kuwa wasanii wakike wanashindwa ku-maintain kwenye game.

Queen Darleen

Darleen amesema kuwa yeye hajawahi kushuka toka enzi hizo na kujifananisha na marehemu Bi. Kidude kuwa mzee wake utaendelea kuwa mzuri hata umri wake ukiendelea kumtupa mkono.

Mimi sijui wao lakini mimi toka  hizo zama za kina Lady Jaydee, akina Ray C mpaka leo hii mimi bado nipo, nakwenda nao level za akina Nandy, yaani mimi nipo humo humo na sitoki yaani na wasitegee kutoka leo, kesho yaani mimi kama bi Kidude nakufa na muziki wangu,“amesema Queen Darleen kwenye mahojiano yake na Wasafi TV.

Kwa upande mwingine, Queen Darleen amezungumzia mavazi yake ambayo mashabiki wake wamekuwa wakimshambulia kuwa anavaa nusu utupu jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Mtanzania.

Kama mimi navaa najiona mwenyewe napendeza, niko fresh, lakini mtu anakuja anakwambia unavyovaa umevaa vibaya hujapendeza? My Friend pesa yangu ambayo nimenunulia nguo mimi unayoniambia sijapendeza, hiyo simu yako uliyoshika gharama yake hazilingani.. Tusipangiane mavazi wala maisha.“amesema Queen Darleeen.

Kuhusu muziki Queen Darleen ameahidi kuachia kazi yake mpya ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa na amewataka mashabiki wake wawe wavumilivu kwani WCB kuna mfumo wa namna ya kuachia ngoma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW