Habari

Mitandao ya kijamii yazimwa kupisha uchaguzi Burundi, Mrithi wa Nkurunziza kupatikana

Mitandao ya kijamii imezimwa huku wananchi wakiendelea kupiga kura nchini Burundi katika uchaguzi mkuu hii leo. BBC imethibitisha kuwa mitandao ya Twitter, Whatsapp na Facebook kuwa haipatikani nchini humo.

Serikali ya Burundi hata hivyo haijalizungumzia suala hilo.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa toka saa 12 asubuhi na vitafungwa saa 10 alasiri.

Wagombea saba wanawania hii leo kumrithi Pierre Nkurunziza, hata hivyo wagombea wawili ndio wanaopigiwa upatu zaidi, kutoka chama cha upinzani CNL Agathon Rwasa na chama tawala CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye.

Raia wa Burundi wanapiga kura ya kumchagua rais, na katika karatasi za kupigia kura, jina la Pierre Nkurunziza halipo.

Siku ya leo inakamilisha utawala wa bwana Nkurunziza ambaye aliingia madarakani katika taifa hilo la Afrika Mashariki miaka 15 iliyopita.

Uchaguzi huo pia unahusisha nafasi za ubunge na madiwani. Matokeo yanatarajiwa kuanzia Mei 25.

‘Mshauri wa ngazi ya juu’

Burundis incumbent president Pierre Nkurunziza (C) reacts to supporters as he arrives to the opening of the campaign of the ruling party

Ijapokuwa anaacha madaraka ya urais, Nkurunziza sasa atakuwa na cheo rasmi kipya cha “mshauri wa ngazi ya juu wa uzalendo.”

Pia atapokea malipo ya $540,000 (£440,000) na makazi ya kifahari. Lakini haijawa wazi ikiwa atatoweka hadharani na kutumia muda wake zaidi kwa mambo mengine mfano mchezo wa soka anaoupenda.

Mchakato wa kuelekea uchaguzi- ambao wagombea saba wamejitokeza kuchua nafasi ya rais- umetawaliwa na gasia na shutuma kwamba uchaguzi hautakua wa haki na huru.

Lakini yoyote kwa atakayeshinda atatakiwa kisheria kupata ushauri kutoka kwa Bwana Nkurunziza juu ya masuala ya usalama na umoja wa kitaifa. Kama watafuata ushauri wake bado halijawa wazi.

Ingawa anaweza kuwashawishi kwa kuonesha mafanikio yake, kama vile kuanzisha elimu ya msingi bure, huduma bure za matibabu kwa wanawake na watoto, na kujenga barabara na hospitali.

Man with a gas maskKulikua na maandamano makubwa wakati Pierre Nkurunziza aliposema kuwa atagombea muhula wa tatu mamlakani mwaka 2015

Miaka mitano iliyopita, muhula watatu wa Bwana Nkurunziza ulianza wakati taifa hilo likiwa katika kipindi cha ghasia za kisiasa. Tangazo lake kwamba angegombea kuwa rais kwa miaka mitano zaidi mamlakani lilichochea hasira ambapo baadhi walihoji uhalali wa hatua hiyo kisheria.

Kulikua na jaribio la mapinduzi, mamia ya watu walikufa katika makabiliano na maelfu wakalazimika kuikimbia nchi yao . Kuchaguliwa kwake mwezi Julai 2015, ambapo alipata karibu 70% ya kura, kulielezewa kama ”mzaha” na kiongozi wa upinzani nchini humo Agathon Rwasa, ambaye alisusia uchaguzi.

Wakati huu , Bwana Nkurunziza aliruhusiwa, baada ya kubadili katiba kugombea tena, lakini anaonekana kuchagua kuishi maisha ya ukimya.

Uchaguzi wakati wa virusi

Uchaguzi wa Jumatano pia umekosolewa kwa kuendeshwa wakati wa janga la virusi vya corona.

Burundi imerekodi visa zaidi ya 40 vya maambukizi ya virusi vya corona, ikiwa na kifo kimoja, lakini busara ya kuendesha mikutano ya kisiasa ya umati wa watu imekua ikihojiwa.

Msemaji wa serikali alisema mwezi Machi kwamba, wakati hakuna visa vilivyokua vimerekodiwa, kwamba nchi imelindwa na Mungu.

Burundi imekataa kuweka sheria kali, huku serikali ikiwashauri tu watu kuzingatia kanuni za usafi na kuepuka mikusanyiko pale inapowezekana-isipokua bila shaka mikutano ya kampeni za kisiasa.

Burundi"s opposition National Freedom Council (CNL), presidential candidate Agathon Rwasa, addresses supporters during a campaign rally in Ngozi province, Burundi April 27, 2020Upinzani pia umekua ukifanya mikutano mikubwa, kama huu

Lakini serikali inasisitiza kuwa waangalizi wa kigeni wa uchaguzi watalazimishwa kutengwa kwa siku 14 kuanzia siku watakapowasili nchini, jambo linaloonekana kama njia ya kuwazuwia kwenda Burundi kabisa.

Uchaguzi unaohojiwa kwa hali ya juu

”Kile tulichokiona katika miezi michache iliyopita ni kwamba fursa ya kisiasa nchiniBurundi ni ndogo ” Nelleke van de Walle, anayefanyakazi katika taasisi ya utatuzi wa migogoro ya Afrika – Central Africa for the Crisis Group think-tank, aliiambia BBC.

“Kwahivyo uchaguzi unaibua maswali juu ya ikiwa utakua wa haki na huru.

Burundi Election Timeline.

“Kutokana na ukweli kwamba hakuna waangalizi wa uchaguzi watakaoruhusiwa nchini kuangalia ni nini kinachoendelea-Ninadhani hiyo inaongeza hatari ya wizi katika uchaguzi, ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu kabla ya uchaguzi pia. .”

Serikali insisitiza kuwa ilionya kuwa kutakua na karantini kwa waangalizi mwezi Aprili ili kuwapa muda

Wanadiplomasia wameelezezea hofu yao juu ya upigaji wa kura nchini Burundi.

Mikutano ya kampeni za kisiasa nchini Burundi inayofanyika wakati wa virusi vya corona imekua ikikosolewaMikutano ya kampeni za kisiasa nchini Burundi inayofanyika wakati wa virusi vya corona imekua ikikosolewa
Presentational white space

Lakini kwa miaka mitano iliyopita, imeweza kubaini njia ya kukabiliana na ukosoaji wa kimataifa ima kwa kukanusha madai ya unyanyasaji dhidi yake au kuamua kuyapuuza. Na kufikia sasa mbinu hizo zimeifaa serikali na chama tawala.

Nchi imeweza kuendelea kwa msaada mdogo wa wahisani, ambao kiasi kikubwa ulitoweka baada ya limbo la kisiasa la mwaka 2015. Matokeo yake, uchaguzi huu wa sasa unadhaminiwa na serikali yenyewe- ukiwa ni wa kwanza katika historia ya Burundi na nadra kuwahi kufanywa barani Afrika.

Yote haya yamewafanya maafisa wa Burundi kujiamini kuwa wanaweza kujifanyia mambo wenyewe.

Bwana Nkurunziza anamuunga mkono mgombea kutoka chama tawala cha CNDD-FDD , Evariste NdayishimiyeBwana Nkurunziza anamuunga mkono mgombea kutoka chama tawala cha CNDD-FDD , Evariste Ndayishimiye
Presentational white space

Miongoni mwa wagombea saba katika uchaguzi wa rais, ni wawili tu wanaoonekana kuwa washindani wakuu.

Bwana Nkurunziza anamuunga mkono mgombea kutoka chama tawala cha CNDD-FDD , Evariste Ndayishimiye, ambaye amekua akishangiliwa katika mikutano mikubwa ya kampeni.

Ni katibu mkuu wa wa chama, waziri wa zamani wa mambo ya ndanina alikua kamanda muasi,samabamba na Bwana Nkurunziza, katika FDD wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivyomalizika 2003.

Wapinzani ‘kuteshwa na kuuawa

Bwana Rwasa, kiongozi wa zamani wa kikundi kingine cha waasi, cha FNL, ametoa wito wa kufanyika kwa “mabadiliko makubwa katika sekta zoteza kitaifa”, alipozungumzana wafuasi wa chama chake cha National Congress for Liberty (CNL), ambacho kilibuniwa mwaka jana.

Licha ya kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha mwaka 2015, alipokua mgombea kwa tiketi ya chama kingine, bado alipata 19% ya kura kwani jina lake lilibaki katika karatasi ya kura.

Wanaume wote hao wawili wanaamini kuwa wana uungaji mkono wa kutosha, lakini imekua ni mapambano kwa Bwana Rwasa. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema serikali imetumia uwezo ilionao kuwatisha na kuzima upinzani pamoja na wafuasi wake.

Bwana Agathon Rwasa "ametoa wito wa kufanyika kwa "mabadiliko makubwa katika sekta zoteza kitaifa"Bwana Agathon Rwasa “ametoa wito wa kufanyika kwa “mabadiliko makubwa katika sekta zoteza kitaifa”
Presentational white space

Kwa mujibu wa Human Rights Watch, kumekua na mauaji 67 yaliyorekodiwa, mkiwemo 14 mauaji yaliyo kinyume na sheria, katika kipindi cha miezi sita. Kumekua pia na matukio ya kutoweka kwa watu, visa vya mateso na kuwakamata watu 200 wanaoangaliwa kama wapinzani wa kisiasa.

Vikosi vya usalama vimeshutumiwa kutumia nguvu kupita kiasi kuzima shughuli za upinzani.

Matumaini ya mwanzo mpya

Tangu ilipopata uhuru kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1962, Burundi imeshuhudia wimbi baada ya wimbi la ghasia baina ya kabila la Wahutu walio wengi na la Watutsi walio wachache

Haijawahi kuwa na kipindi cha kudumu cha amani baada ya mabadiliko ya kiongozi wake.

Melchior Ndadaye, ambaye ni Muhutu, alichaguliwa kua rais katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 1993.

Lakini matumaini ya kukita mizizi ya demokrasi yaliondoshwa miezi mitatu tu ya urais wake, wakati kundi cha askari walioongozwa na jeshi la kabila la Watutsi kumuua pamoja na mawaziri kadhaa na washirika wake wa kisiasa.

Unaweza pia kusoma:

 

Makundi ya waasi wa Kihutu Hutu FDD na kile cha Bwana Rwasa FNL, wakati huo yalichukua silaha katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muongo, na kusababisha vifo vya watu wapayao 300,000.

Vurugu za 2015 zilimaliza kipindi kingine cha amani kiasi. Lakini swali ni ikiwa rais ajae anaweza kurejesha sifa ya nchi machoni mwa waangalizi wa kimataifa

Bwana Nkurunziza, aliyejihami kwa cheo cha “mshauri wa ngazi ya juu wa uzalendo “, anaweza kutumaini kuendelea kuendeleza kiasi fulani cha ushawishi.

Lakini hata kama mgombea wa chama chake atashinda, hilo halina hakikisho kuwa ataendelea kuongoza kama atataka kufanya hivyo.

Nchini Angola, rais wa muda mrefu Jose Eduardo dos Santos alitarajia kuendelea kuwa na usemi katika serikali baada ya João Lourenço kuchukua nafasi yake mwaka 2017.

Lakini kumteua mrithi wake kulikua na athari dhidi yake, kwani aliwafuta kazi na hata kuwashitaki baadhi ya watoto wa Bwana Dos Santos na washirika wake wa karibu.

Benki ya dunia inakadiria kuwa saba kati ya warundi 10 wanaishi chini ya mtari wa umaskini, na Warundi milioni 11 watatumai kwamba yeyote atakayeishia kuwa rais atayafanya maisha yao kuwa bora.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents