Habari

Mkurugenzi wa FBI Wray: China ni tishio kubwa kwa Marekani, imeanza kuipiku kuwa taifa lenye nguvu

Mkurugenzi wa shirika la FBI nchini Marekani amesema kwamba vitendo vya upelelezi na wizi unaotekelezwa na serikali ya China ni tishio la muda mrefu kwa Marekani.

Akizungumza katika Taasisi ya Hudson mjini Washington, Christopher Wray alielezea kampeni ya usumbufu iliyokithiri.

Alisema kwamba China imeanza kuwalenga raia wa China wanaoishi ughaibuni, ikiwashurutisha kurudi nyumbani na kwamba ilikuwa inajaribu kuingilia utafiti wa corona wa Marekani.

”China imeanza juhudi za kuhakikisha kuwa ndio taifa la pekee litakalokuwa na uwezo mkubwa zaidi duniani kwa hali na mali”, aliongezea.

Katika hotuba iliochukua karibia saa moja siku ya Jumanne, Mkurugenzi wa FBI alielezea jinsi China inavyoingilia masuala ya Marekani kupitia kampeni kubwa ya upelelezi wa uchumi wa Marekani, wizi wa data na fedha kwa lengo la kushawishi sera za Marekani.

”Tumefikia wakati ambapo FBI sasa imeanza kufungua kitengo cha kukabiliana na visa vya Ujasusi wa China kila baada ya saa 10”, bwana Wray alisema.

”Kati ya visa 5000 vya kukabiliana na ujasusi vinavyoendelea kote nchini , karibia nusu yake vinahusishwa na China”.

Mkurugenzi huyo wa shirika la ujasusi nchini Marekani alisema kwamba rais wa China Xi Jinping alianzisha mpango kwa jina ‘Fox Hunt’, unaowalenga raia wa China ughaibuni wanaoonekana kuwa tishio kwa serikali ya China.

”Tunazungumzia kuhusu wapinzani wa kisiasa, watoro na wakosoaji walio na lengo la kufichua ukiukaji wa haki za kibinadamu unaotekelezwa na China”, alisema.

”Serikali ya China inataka kuwalazimisha kurudi nyumbani na mbinu zinazotumiwa na china kufanikisha mpango huo inashtua”.

Aliendelea: inaposhindwa kumpata mtu inayemtafuta, serikali ya China hutuma mjumbe kutembelea familia ya mtu huyo nchini Marekani. Ujumbe unaotolewa ni : Rudi China haraka ama jiue.

Washington sasa inaiona Beijing kama mshindani wa

Uchambuzi na mwandishi wa BBC Zhaoyin Feng, Washington

Hii sio mara ya kwanza kwa mkurugenzi wa FBI Christopher Wray kuiorodhesha China kama tishio kubwa la kijasusi kwa Marekani, lakini siku ya Jumanne alizungumzia kuhusu jinsi Bejing inavyofanya juhudi kuwa taifa la pekee lenye uwezo mkubwa duniani.

”Hii ni ishara kwamba Washington inaiona Bejing sio tu kama mpinzani mkali, lakini pia mpinzani anayetaka kuongoza ulimwengu”.

Tangu mlipuko wa virusi vya Covid -19 nchini Marekani, utawala wa rais Trump umeishutumu China kwa jinsi ilivyokabiliana na mlipuko huo, upelelezi wake wa kiuchumi na sheria mpya ya usalama mjini Hon Kong.

Matamshi ya bwana Wray ni miongoni mwa msururu wa hotuba kali iliotolewa na afisa mkuu wa Marekani kuhusu suala hilo.

Serikali ya bwana Trump inasema kwamba ni wakati kuamka na kutoka katika miaka 40 ya sera zilizofeli kuhusu China, huku wakosoaji wakiliona hilo kama jaribio kumuonolea lawama raistena Trump kuhusu mapungufu yake ili kuimarisha nafasi yake ya kuchaguliwa kwa awamu ya pili.

Kilicho wazi ni kwamba vita vya kupigania uongozi kati ya Uchina na Marekani vimebadilika kimsingi, na haijalishi ni nani atakaye kuwa rais baada ya uchaguzi mkuu wa Marekani, msimamo mkali wa mahusiano kati ya China na Marekani utazidi kuendelea.

Katika hotuba isio ya kawaida , bwana Wray aliwataka raia waliozaliwa China lakini wanaoishi Marekani kuwasiliana na FBI iwapo watalengwa na serikali ya China ikiwataka kurudi nyumbani.

Serikali ya China imepinga mpango huo siku za nyuma , ikisema ni juhudi halali za kukabiliana na ufisadi.

”Tishio linalotolewa na China litaangaziwa zaidi katika hotuba ya mwanasheria mkuu pamoja na waziri wa masua laya kigeni nchini Marekani katika kipindi cha wiki chache zijazo”, alisema bwana Wray. Hotuba hiyo inajiri wakati ambapo kuna hofu kati ya China na Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump ameikosoa pakubwa China kufuatia mlipuko wa corona akililaumu taifa hilo kwa kusababisha janga hilo.

Katika hatua nyengine Mike Pompeo amesema kwamba utawala wa Trump unafikiria kupiga marufuku programu za China -ikiwemo ile ya Tiktok ilio na umaarufu mkubwa. Programu hizo “zinatumika kukipelelezea Chama cha Kikomyunisti cha China”, alisema.ke

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents