Fahamu

Mtoto wa baba wa taifa Makongoro Nyerere asimulia alivyosahaulia kwenye vita Uganda – Video

Mtoto wa baba wa taifa Makongoro Nyerere asimulia alivyosahaulia kwenye vita Uganda - Video

Mtoto wa baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere, Bw Makongoro Nyerere asimulia alivyosahauliwa na baba yake ambaye alikuwa Rais wa awamu ya kwanza Marehemu Mwl Julius Kambarage Nyerere kwenye Vita ya Uganda na Tanzania mwaka 1978.

Ikumbukwe nchi ya Uganda kipindi hicho ilikuwa ikiongozwa na Nduli Idd Amini Dada.
Akitoa simulizi hiyo nyumbani kwa Baba wa taifa wakati alipoenda kutembelewa na wasanii kwa ajili ya kuzindua Tamasha la Mwl Nyerere Festival linalotarajiwa kuanza siku ya ijumaa hii katika Ukumbi wa Mwl Nyerere Posta huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
Makongoro ametoa simulizi hii akiulinganisha Uongozi wa baba wa taifa na Uongozi wa sasa hivi uliopo chini ya Dkt. Magufuli kuwa anafuata sheria na haangalii mtoto wake wala ndugu yake bali yeye anafuata sheria za nchi na ndio maana yeye aliachwa Uganda na alishindwa kupata msaada wa baba yake kwa kuwa sheria ilitaka vijana wote wa JKT walioko kwenye kambi za Jeshi waende Vitani na alikaa karibia mwezi mzima bila baba yake kujua yuko wapi.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents