Habari

Mtumishi serikalini akamatwa na jeshi la polisi kwa kuchochea maandamano

Jeshi la polisi mkoani Dodoma limemkamata na mfanyakazi mmoja wa mfuko wa afya wa NHIF kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kwenye mitandao ya kijamii yanayoratibiwa na mwanamke maarufu mitandaoni ajulikanaye kwa jina la Mange Kimambi.

Tokeo la picha la Gilles Muroto
Kamanda Gilles Muroto

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 21, 2018, Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi Mwandamizi, Gilles Muroto amesema jeshi hilo limemshikilia mtumishi huyo wa NIHF na mwenzake mkazi wa Bahi kwa makosa ya kuchochea maandamano.

Akitaja majina ya waliyoshikiliwa Kamanda Muroto amesema kuwa ni AMANI CHARI, ambaye ni mfanyakazi wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya – NHIF na Yuda Mbata ambaye ni mkazi wa wilayani Bahi.

Kwa upande mwingine, Kamanda Mruto amewaonya watu kutofuata mkumbo wa kuhamasisha maandamano iwe kwa njia ya mitandao au njia yoyote ile kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents