Burudani

Mwanadada Faith Rogers ampandisha R. Kelly kizimbani kwa kudai kuwa alimuambukiza gonjwa la zinaa wakati wa mahusiano yao

Kufuatia sakata la kuwarubuni wasichana wadogo kingono,linalomkabili nguli wa muziki wa R&B Marekani na Duniani kote Robert Sylvester Kelly alimaarufu R Kelly, limezua sura mpya tena.

Hii ni baada ya Mwanamuziku huyo kupandishwa kizimbani hivi karibuni kutokana na shtaka lake dhidi ya mwanadada “Faith Rogers”, ambaye alimfikisha kwenye mikono ya sheria akidai kubakwa na kuambukizwa ugonjwa wa zinaa mwaka 2017 na nguli huyo wa muziki nchini Marekani.

Kwa mujibu wa jarida la MSN Entertainment, Kwenye shitaka hilo la mwezi Mei mwaka jana, Faith amedai kuwa R. Kelly alimlazimisha kufanya mapenzi bila ridhaa yake na kisha kumuachia ugonjwa wa zinaa (herpes) kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 19.

Ijumaa wiki iliyopita, wakili wa msichana huyo, Bi. Lydia Agu aliitisha mkutano na waandishi wa Habari kutangaza kurejea kwa shauri hilo ambalo limedumu kwa miezi 7 sasa. Lakini Wawili hao walidumu kwenye mahusiano kwa mwaka mmoja.

Anasema kuwa wakati wa uhusiano wao wa muda mrefu, ulioanza wakati alipokuwa na umri wa miaka 19, alikuwa akifungiwa ndani kwa muda wa saa nzima ” na anasisitiza kuwa ni mtu ambaye Faith alifaa kumuita baba”.

Katika barua hiyo, mtu anayejitambulisha kama R Kelly aliandika kwamba ikiwa shitaka litaendelea, angekuwa na “mashahidi 10 wa kiume” ambao wangetoa ushahidi kuhusu maisha ya ngono ya Bibi Rodgers. Alisema atapaswa kuacha kama kutoa ushahidi huo endapo mwanadada huyo angejali sana sifa yake mwenyewe”

Barua hiyo ilisema mwimbaji pia anahitaji nyaraka za matibabu ya madai yake kwamba alimpa ugonjwa wa ngono yaani (herpes).

Mwanasheria wa mwimbaji, Steve Greenberg, alidai barua hiyo “inaonekana bandia” na Kelly anakataa kosa lake. “Yeye haandikagi barua,” alisema.

Barua hiyo ilitumwa wiki chache baada ya mwimbaji huyo kutuhumiwa na mashtaka ya kumtukana Ms. Rodgers na kumuita “
“non-permissive, painful and abusive sex””. Sasa, Ms Rodgers ana umri wa miaka 21,

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents