Habari

Mwanamke aliyehongwa laki mbili auawa kikatili baada ya kukataa kushiriki tendo la ndoa

Mwanaume mmoja nchini Thailand anashikiliwa na jeshi la polisi nchini humo kwa kosa la kushambulia na kuua watu wawili mtu na mama yake kwa kuwachoma kisu.

Mtuhumiwa wa mauaji, Hasan Jehha akiwa mikononi mwa polisi.

Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la Hasan Jehha (30) alitekeleza mauaji hayo nyumbani kwake baada ya kumualika mwanake huyo wikiendi iliyopita kumtembelea kijijini kwao Moo 5 mjini Tambon Kalisa katika wilaya ya Rangae.

Kwa maelezo ya mtandao wa gazeti la Bangkok Post la nchini humo limeeleza kuwa Jehha alikuwa na mahusiano na mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Bismee Sulong kutoka katika mji jirani wa Cho Airong kwa muda mfupi na alikubali kumsaidia kiasi cha Thai Baht 1,650/=  sawa na Tsh laki 2 alichokuwa anadaiwa kwa ajili ya kulipia pango.

Polisi mjini Tambon Kalisa wamethibitisha tukio hilo ambapo wamesema mtuhumiwa alitenda tukio hilo jumamosi iliyopita.

“Tunamshikilia mwanaume mwenye umri wa miaka 32 kwa kosa la mauji ya watu wawili mwanamke wa miaka 27 na mtoto wa miaka minne aliyotekeleza tarehe 11 Novemba, 2017 katika mtaa Moon 5, wilayani Rangae .”amesema Kamishna wa jeshi la polisi mjini Rangae, Pol Lt-General Ronnasilp Phusara.

Polisi wamesema miili ya watu hao wawili iliokotwa darajani katika kijiji hicho na wasamalia wema waliokwenda kutoa taarifa polisi, kabla ya uchunguzi wa kutumia kamera za CCTV kutumika na kumbaini Jehha kuhusika na tukio hilo.

Ndugu wa mwanamke huyo wanasema siku ya ijumaa aliwaaga kuwa anakwenda kwa rafiki yake na mtoto wake na kuahidi kuwa angerudi siku hiyo hiyo lakini cha ajabu hakurudi siku hiyo.

Hata hivyo, mtuhumiwa amekiri kutekeleza mauaji hayo na kujitetea kuwa wote wawili walikuwa wamelewa na ilitokea wakati akimlazimisha kufanya mapenzi.

Mtuhumiwa atapandishwa kizimbani jumatano kusomewa mashtaka ya kesi ya kuua kwa kukusudia ambapo kama atakutwa na hatia basi hukumu yake kwa mujibu wa sheria nchini humo ni kunyongwa hadi kufa.

Chanzo:BangKok Post

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents