DStv Inogilee!

Mwanamuziki maarufu nchini Rwanda aliyewahi kupanga njama ya kumuua Rais Kagame, atoka gerezani

Rais Paul Kagame wa Rwanda ametoa msamaha kwa mwanamuziki maarufu nchini humo, Kizito Mihigo na kiongozi wa upinzani, Victoire Ingabire Umuhoza waliokuwa wamefungwa gerezani tangu mwaka 2013 na 2015.

Kizito Mihigo

Tamko la serikali lililotolewa Ijumaa jioni limeeleza kuwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri ulioendeshwa na Rais Kagame jana Jumamosi, umepitisha kuachiwa kwa wafungwa 2,140 waliokuwa wanastahiki msamaha huo chini ya vifungu husika vya sheria.

Victoire Ingabire Umuhoza

Kwa mujibu wa kifungu cha 109 cha Katiba ya Rwanda kinasema kuwa “Rais wa Jamhuri ya Rwanda ana uwezo wa kutumia mamlaka aliyopewa kutoa msamaha kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na sheria na baada ya kushauriana na Mahakama ya Juu”.

Mwaka 2013 Ingabire alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 15 na Mihigo alifungwa miaka 10 mwaka 2015 kwa makosa ya uhaini.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW