Habari

Mwanaume akatwa sehemu za siri na mwanamke kwa kushindwa kulipia T sh 5000 kwa mshindo mmoja – Video

Mwanaume akatwa sehemu za siri na mwanamke kwa kushindwa kulipia T sh 5000 kwa mshindo mmoja - Video

Jeshi la Polisi mkoani Mara linamshikilia mwanamke anayefahamika kwa jina la Marusi Samweli kwa tuhuma za kumjeruhi mpenzi wake kwenye uume kwa kumkata na wembe.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Daniel Shillah amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia tarehe 10 ya mwezi Jnuari katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Mugumu wilayani Serengeti.

ambapo Mwanamke aitwaye Nyangi Ismael amekatwa kwa tuhuma za kumkata sehemu za siri Mpenzi wake Joseph Nyanakwi wakiwa Gesti baada ya kushindwa kumlipa Tsh.Elfu 5 walizoahidiana kulipana kwa kila mshindo mmoja wakati wa tendo la ndoa.

Akiongea mwanaume huyo amesema kuwa:-

“Tulianza vinywaji tukakubaliana kila mshindo Elfu 5 akaomba kwanza Elfu 20 nikampa, tumelala kila nikimaliza mzunguko nikawa nalipa Elfu 5, mitatu nililipia Elf 15 lakini huu wa nne nikamwambia kata kwenye ile Elfu 20 akagoma”

“Kumbe alikuwa na wembe ghafla Alfajiri akashika uume wangu na kuanza kuukata kuanzia chini kwenye korodani nilipambana lakini akawa ameshaniumiza vibaya”

Katika tukio lingine, Juma Waryoba maarufu kama (Kisangura) 27, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumchoma na kisu mara kadhaa mwilini kwake.

Shillah ameongeza kuwa tukio hilo limetokea wilayani Butiama ambapo mwanaume huyo anatuhumiwa  kumuua mke wake kwa kuchoma na kisu na kisha kutoroka kusikojulikana huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda ametoa wito kwa wananchi wa mko wa Mara kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani kama kuna migogoro ndani ya familia ni vizuri kuitatua kwa njia ya mazungumzo na sio kutumia nguvu, akisema kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya Jamuuri ya Muungano wa Tanzania.

https://www.instagram.com/p/B7LPXpZh-eK/

Eatv.Tv.

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents