Burudani

Mzee Yusuf: Nimeshachoka kuwa mwanamuziki wa Tanzania pekee

Staa wa muziki wa Taarab, Mzee Yussuf amesema tayari ameshafanya yote makubwa katika muziki wake hapa nyumbani hivyo anaanza kutanua muziki wake kimataifa zaidi.

Mzee Yusuf

Muimbaji huyo aliyeshoot video ya wimbo wake mpya Hewala aliomshirikisha Vanessa Mdee nchini Afrika Kusini, ameiambia Bongo5 kuwa kazi hiyo anaihesabu kama ndiyo kazi yake ya kwanza katika safari yake ya mafanikio.

“Tayari kila kitu nimeshafanya hapa nyumbani na Tanzania inanitambua,” alisema.

“Nimesema niache hapo nilipoishia nianze moja. Nimeshachoka kuwa mwanamuziki wa Tanzania pekee, nimechoka sana. Kwa sababu Tanzania peke yake haitoshi kukusogeza katika biashara ya soko la dunia. Mimi najua nikiwekeza pesa kwa kufanya kazi nzuri, wimbo mzuri wa mduara au Taarab pamoja na video vitaenda na vikienda ndiyo thamani yangu itaongezeka kwa sababu nimewekeza pesa ili kupata kazi nzuri. Lazima tutoke nje ili tuwape changamoto maproducer wetu kwa sababu mimi nimewaangalia watayarishaji wa muziki wa Afrika Kusini sio vitu wanavyotumia ni vya kwao wamekodi, sema wao wanajiongeza kwanini sisi tushindwe?. Kwahiyo mashabiki wa muziki wangu wakae tayari hii kazi itatoka siku yangu ya kuzaliwa, January siku za mwanzo,” alisema Mzee Yussuf.

Mzee Yusuf pia amesema yupo kwenye mazungumzo ya kolabo na wasanii wa Kenya wakiwemo Sauti Sol.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents