Habari

Nabii aliyeahidi kumfufua kaburini marehemu aliyefariki siku nne ashikwa na polisi baada kushindwa (+video)

Nabii aliyeahidi kumfufua marehemu kaburini aliyefariki siku nne ashikwa na polisi baada kushindwa (+video)

Ukistaajabu ya Musa kwa dunia hii basi bila shaka utajionea ya firauni kwani kumekuwa na Manabii wengi kiasi kwamba wakristo wanaamini huenda hizi ni nyakati za mwisho.

Prophet In Police Net After Failing To Resurrect Corpse
Nabii Getayawkal Ayele akiwa mikononi mwa Polisi

Sasa Nabii mmoja aitwaye Getayawkal Ayele kutoka nchini Ethiopia amekamatwa na polisi nchini humo baada ya kuahidi kumfufua marehemu aliyefariki siku nne zilizopita huko mjini Galilee kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa YPRESS Hausa wa nchini Ethiopia umeeleza kuwa Nabii Ayele aliiahidi familia ya marehemu aliyetambulika kwa jina la Belay Bifu  kuwa atamfufua ndugu yao kama Yesu alivyofanya kwa Lazaro.

Nabii huyo kwenye video iliyovuja mtandao anaonekana akimuuita marehemu ‘Belay Belay’ na kulala juu ya jeneza kwa dakika moja lakini Marehemu hakuweza kuitika.

Ndugu na wananchi waliofika kwenye kaburi hilo ambalo lilifukuliwa kwa ajili ya miujiza hiyo walianza kumshambulia kwa mawe Nabii Ayele na ndipo Polisi walipofika eneo la tukio na kumkamata Nabii huyo kwa ajili ya usalama wake na mahojiano zaidi.

Tukio hilo limetokea Ijumaa ya wiki hii na Kamanda wa Polisi mjini Tadese Galilee kupitia BBC Hausa amethibitisha kumshikilia Nabii huyo. Tazama video yote ya  tukio hilo  hapa chini

https://youtu.be/rVUdgDKDCuI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents