Tupo Nawe

Naibu Waziri wa Elimu Ole-Nasha, atoa maagizo NACTE ya kuvifutia usajili Vyuo hivi

Naibu Waziri wa Elimu Ole-Nasha, atoa maagizo NACTE ya kuvifutia usajili Vyuo hivi

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia William Ole-Nasha, ameliagiza Baraza la Taifa la Elimu na ufundi (NACTE) kuvifutia usajili vyuo vyote vinavyosajili wanafunzi feki.

Pia alitaka baraza hilo, kuvichukulia hatua kali vyuo ambavyo vinavyochelewesha matokeo ikiwa ni pamoja na kuvifungia.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea ofisi hizo, anasema kuwa Sheria zifuatwe ili vyuo visiwe vikwazo kwa wanafunzi kushindwa kusonga mbele.

“Inatakiwa kuangalia ubora wa wanafunzi kuna vyuo vinavyosajiliwa kiholela mwishoni mwanafunzi anakuja kugundua kuwa hana sifa, Ukigundua chuo kama hicho chukua hatua kali pamoja na kufuta usajili wa hicho chuo, hata kama nicha serikali hakikisheni vyuo vinachukuwa wanafunzi wenye sifa stahiki.

“Ucheleweshaji vyeti unaathiri wanafunzi wanafunzi pamoja na wazazi, kujenga mitaara mizuri ya kujiajiri mwenyewe na wanaopenda kuajiliwa waweze waajirike”amesema Ole Nasha.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW