Burudani

Namuomba Mungu aniumbe upya-Aeleza kwa majonzi mrembo aliyepata upofu kwa kubadilisha rangi ya macho

Mwanamitindo maarufu nchini Argentina ambaye kazi zake kwa sasa anafanyia nchini Marekani, Nadinne Bruna amejikuta akimuomba Mungu usiku na mchana amfanyie miujiza aweze kuona tena baada ya kuharibu macho yake kwa kufanya upasuaji mdogo wa kubadilisha rangi ya macho yake.

Nadinna kabla ya kufanya upasuaji wa kubadilisha rangi ya macho.

Nadinne (32) amesema kuwa alifanya maamuzi ya kubadilisha macho yake kwa lengo la kubadili muonekano wake lakini tangu afanye hivyo mwaka 2016 mwezi Desemba hadi leo macho yanamuuma na anazidi kupoteza uwezo wa kuona.

The model slipped into a deep depression throughout the past two years, but said she was lucky to have the support of her sister
Nadinne

Mwanamitindo huyo aliyejivunia umaarufu mkubwa nchini Argentina amesema kuwa hata picha anazochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram ni za zamani na anasaidiwa na meneja wake kuposti.

Ms Bruna, who has 198,000 followers on Instagram, has been left with irreversible damage to her eyes that has 'f***** up' her life and left her depressed

Ukurasa wake wa Instagram una followers wapatao 198k na tayari umeshatambuliwa (Verified).

Akizungumza na mtandao wa Canal City TV wa nchini Colombia, Nadinne amesema ameondoka Miami hadi Colombia wiki iliyopita baada ya kutafuta mtaalamu mwingine mtandaoni ambaye anaamini kuwa atamsaidia ingawaje bado hali yake ni mbaya hajapata nafuu.

Daktari wangu wa kwanza aliyenifanyia upasuaji hadi leo ameshindwa kabisa kunitibu nirudi hali yangu ya zamani, Mpuuzi sana nakosa matangazo ya kibiashara niliyokuwa nafanya zamani kwani macho yangu yamekuwa mekundu na yanaogofya. Nimetafuta kila namna lakini nashindwa nimepata dawa na ushauri kutoka kwa wataalamu lakini hali yangu ndio kama unavyoniona, Namuomba Mungu tu aniumbe upya kwani napata maumivu makali sana,“amesema Nadinne.

Nadinne kushoto kwenye picha

Kwa upande mwingine, Naddine amesema kuwa tayari ameshachukua hatua za kisheria dhidi ya Daktari huyo aliyemfanyia upasuaji wa kwanza kwa kuwasilisha malalamiko yake kwa Idara ya  Chakula na Madawa nchini Marekani.

Unaweza ukacheki picha na video zake zaidi kwenye ukurasa wake wa Instagram hapa chini;

https://www.instagram.com/p/Bhbu0YgBsOn/?taken-by=nadinne.bruna.model

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents