Habari

Ninaendelea kumuombea Mh. Lissu apone haraka maumivu anayopitia – Waziri Ummy

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema anaendelea kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu apone haraka majeraha na maumivu yote anayoyapitia.

Waziri Ummy kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema huku akimhakikishia Mbunge huyo kuwa serikali ipo tayari kugharamia matibabu yake.

1/2 Kuhusu Matibabu ya Mhe Tundu Lissu – ninaendelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu apone haraka majeraha na maumivu yote anayopitia.

2/2 Nimuhakikishie Mh Lissu na familia kuwa Serikali ipo tayari kugharamia matibabu yake zaidi pindi tu tutakapopata maombi kutoka kwao

Mbunge Lissu alijeruhiwa Septemba 7 mwaka huu eneo la ‘area D’ mjini Dodoma na watu wasiojulikana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents