Aisee DSTV!

Ningemshauri Harmonize aoe, Mimi ndio nimefanya watu wote Kisarawe wampende – DC Jokate

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo amedai kuwa yeye ndiye aliyewafanya watu wengi kwenye wilaya yake wampende msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize. Kwani amekuwa akitumia nyimbo zake kwenye matukio mbalimbali ya kijamii.

Harmonize na DC Jokate

Jokate ameeleza hayo jana Mei 25, 2019 kwenye Futari iliyoandaliwa na Harmonize Wilayani Kisarawe, ambayo ililenga msanii huyo kufuturisha mashabiki wake waliopo wilayani humo.

Mimi actually ndio nimefanya watu wengi wilayani kwangu wampende Harmonize, Sasa hivi wimbo ambao tunaupenda ni Kainama na Kwangaru, Na sio unafiki sisi nyimbo zake tunazitwanga sana, maana yake ukiingia field lazima upige muziki kidogo. Sisi Kwangwaru, Kainama na hii Never Give Up tunaisikiliza kwa sababu inaamsha.” amesema DC Jokate.

Kwa upande mwingine, Jokate amemshauri Harmonize aoe na pia amekaribisha ndani ya wilaya yake kwenda kuwekeza kwani fursa zinapatikana kwa wingi.

Mimi nilitaka nisema aoe lakini nakumbuka mimi mwenyewe sijaolewa, Namshauri mimi awekeze Kisarawe kuna ardhi ya kutosha,” amesema Jokate.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW