Nipo single, wanaume wengi wanakuja nikiwakubalia wiki moja wananikimbia-Anne Kansiime

Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Uganda, Anne Kansiime amesema kuwa bado hajakata tamaa ya kutafuta mwanaume atakayemuoa ingawaje amekuwa akipata majaribu makubwa kwenye maisha yake upande wa mahusiano.

Anne Kansiime

Mchekeshaji huyo tangu mwaka jana wamwagane na mchumba wake wa muda mrefu, Gerald Ojok amesema kuwa tangu kipindi hicho amekuwa akitongozwa na wanaume wengi lakini kila aliyemkubalia hakukaa na yeye muda mrefu.

Kansiime amedai kuwa wanaume wengi aliowapata wamekuwa wakimtoroka ndani ya wiki na wengine wamekuwa wakimuacha bila hata kutoa sababu.

“Nipo single, ila sio mpweke, nimekuwa nikipata maombi mengi ya wanaume wengine nawakubalia lakini ndani ya wiki moja wananikimbia tena wengine bila hata kutoa sababu, sijui tatizo nini?”amesema Kansiime kwenye mahojiano yake na kituo cha runinga cha NTV cha nchini Kenya katika kipindi cha The Trend.

Hata hivyo, Kansiime amedai kuwa bado anamuomba Mungu na hachoki kwani anaamini kuwa kuna mwanaume ambaye wataendana naye na atamuoa.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW