Habari

Nyumba aliyokuwa amehifadhiwa MO Dewji kipindi ametekwa yapatikana, Jeshi la Polisi lakamata watuhumiwa 40 (+Audio)

Leo Jeshi la Polisi mkoani Dar Es Salaam limeionesha nyumba aliyokuwa amehifadhiwa mfanyabiashara MO Dewji kipindi alivyokuwa ametekwa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Novemba 11, 2018 Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam ameionesha nyumba hiyo na kueleza kuwa watu 40 wameshikiliwa kufuatia tukio hilo.

Nyumba hiyo ambayo inapatikana maeneo ya Mbezi Beach Jijini Dar Es Salaam, inaelezwa kuwa ndiyo aliyokuwa amehifadhiwa Mo Dewji kuanzia Oktoba 11 siku aliyotekwa hadi Oktoba 20 siku aliyoachiwa na watekaji hao.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents