P-Funk ‘Majani’ apata mtoto wa kiume, Mastaa na viongozi wa serikalini wampongeza

Mkurugenzi wa Studio za Bongo Records P-Funk ‘Majani’, leo Julai 22, 2018 mapema asubuhi amefanikiwa kupata mtoto wa kiume.

Akithibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Majani amesema amepata mtoto wa kiume na jina lake ni Parees P Matthysse.

Kufuatia tukio hilo baadhi ya mastaa na viongozi wa serikalini wamejitokeza kumpa pongezi kwa kuujaza ulimwengu.

lilommy: Mzeeeee…. Hongera Sana @majani187 God bless you and your family.
hamisi_kigwangalla: Hongera sana bro. Mungu amkuze salama na maisha yake yawe yenye faida kwa ulimwengu! 🙏🏿 @majani187
mwanafa: Hongera bro..hili wazo la @therealfidq sio baya nalo ukiliangalia kwa undani
monalisatz: Hongera sana
gentriez: Oi Hongera sana Big
therealfidq: Hongera sana mkuu.. @majani187 sasa si tuchome nyama tu badala ya kwenda beach?
fredwaatz: blessings brother

Mtoto wa Majani amezaliwa zikiwa ni siku tatu tu zimepita tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda naye apate mtoto wa kiume.

Related Articles

2 Comments

  1. Na atarajie kupata mjukuu kupitia kwa mtoto wake aliyezaa na aliyekuwa ‘waifu’ wake Kajala maana naona binti keshakuwa mkubwa hivi sasa na mama yake huwa ‘anamtupia’ sana humu mitandaoni!

Bongo5

FREE
VIEW