DStv Inogilee!

PIGO KWA CHADEMA: Mhe. Lowassa arudi CCM, Rais Magufuli ampokea kwa ujumbe mzito (+video)

Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa leo Ijumaa Machi Mosi, 2019 ametangaza uamuzi wa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mzee Lowassa amerejea katika chama chake cha zamani shughuli iliyofanyika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Uamuzi wa Lowassa kutangaza kurejea CCM ameuchukua ikiwa imepita miaka mitatu tangu alipotangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema Julai 28, 2015 baada ya jina lake kukatwa katika mchakato wa kuwania urais mwaka 2015.

Mhe. Lowassa alikuwa mgombea wa urais wa Chadema mwaka 2015, akiungwa mkono na vyama vya Ukawa vya Chadema, NLD, CUF na NCCR-Mageuzi .

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW