Habari

Prof. Mkenda : Fursa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu yaongezeka wafikia 252,245

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema ili kuwezesha na kuimarisha huduma ya utoaji na upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu wenye sifa na uhitaji, Serikali itaongeza fursa za mikopo hiyo kwa wanafunzi hao kutoka 223,201 hadi 252,245.

Hayo yamebainishwa leo bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2024/2025.

Prof. Mkenda amesema serikali itatoa mikopo kwa wanafunzi 84,500 wa mwaka wa kwanza ambapo shahada ya kwanza 80,000, shahada za juu 2,000, wanaosoma nje ya nchi 500 na Samia Skolashipu 2,000, aidha itatoa mikopo kwa wanafunzi 157,745 wanaoendelea na masomo.

“Serikali itatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 40 wenye ufaulu wa juu kwenye masomo ya sayansi hususan wanafunzi wa kike waliohitimu Mtihani wa Taifa ya Kidato cha Sita na shahada ya awali kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),” amesema na kuongeza

“Itaendelea kukusanya madeni ya mikopo iliyoiva ya kiasi cha Shilingi Bilioni 198 kutoka sekta ya umma na kuimarisha makusanyo kutoka sekta binafsi na isiyo rasmi. Aidha, itatafuta wanufaika wapya 40,000 wenye marejesho ya mikopo iliyoiva ikijumuisha wanufaika wapya 5,000 wenye mikopo chechefu kutoka sekta binafsi na isiyo rasmi; na itaanza kutoa ufadhili kwa ajili ya shahada za juu ikiwemo eneo la fani ya mionzi na nyuklia,” amesema

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents