Habari

Q Jay apandwa na kichaa, Makamua awaomba Watanzania wamsaidie kuokoa maisha yake

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Q Jay ambaye aliwahi kutamba na kibao cha Sifai imeelezwa kuwa kwa sasa hali yake kiakili haipo sawa.

Akiongea na Bongo5 rafiki wa karibu na msanii huyo, Makamua amesema kuwa kwa sasa Q Jay yupo Bukoba na kwasasa amekuwa kama chokaraa kwani amekuwa anaokota makopo na kuongea vitu visivyoeleweka.

Akielezea chanzo hasa cha tatizo hilo, Makamua amesema kuwa ni kutokana na ugumu wa maisha pia na msongo wa mawazo kutokana na kuachana na familia yake.

Kwa upande mwingine Makamua amewataka Watanzania wamchangie kwa chochote kile ili aweze kupata matibabu ya haraka, kwani Madaktari wamemueleza kuwa anahitaji msaada wa ushauri na nasaha kutoka kwa watalaamu wa Saikolojia.

Makamua amesema kwa sasa jitihada zinazofanyika ni kumsafirisha kutoka Bukoba kuja Dar es salaam kwanza kwa ajili ya matibabu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents