Habari

Raia mmoja kutoka nchini India afungwa maisha jela kwa utekaji feki wa ndege, fahamu ilivyokuwa

Raia mmoja kutoka nchini India afungwa maisha jela kwa utekaji feki wa ndege, fahamu ilivyokuwa

Mfanyabiashara mmoja wa kihindi amefungwa kifungo cha maisha jela baada ya kuweka waraka feki kwenye choo cha ndege ya kampuni ya India-Jet Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka New Delhi kuelekea Mumbai. Birju Salla alisema kuwa alitegemea kuwa ndege hiyo ingefunga safari zake na hivyo mpenzi wake anayefanyia kazi kampuni hiyo angelazimika kuacha kazi ya kuwahudumia wasafiri katika kampuni hiyo angeacha kazi na kuishi nae mjini Mumbai.

Kwa mujibu wa BBC. Bwana Salla pia amepigwa faini ya rupia milioni 50 sawa na dola 720,725. Salla ndiye mtu wa kwanza kushtakiwa chini ya sheria mpya ya India zinazozuwia utekaji nyara. Chini ya sheria hiyo anayepatikana na hatia ya utekaji anakabiliwa na kifungo cha maisha jela au ,hata kunyongwa.

Mfanyabiashara huyo alikiri kuwa aliandika waraka huo wa tisha la ugaidi na kuuchapisha katika ofisi yake iliyopo mjini, kabla ya kuelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya safari yake mwezi Oktoba 2017.

Waraka huo ulisema kuwa watekaji 12 na vilipuzi kadhaa vilikuwa ndani ya ndege na kuamrisha kwamba ndege hiyo ielekezwe kwenye jimbo la Pakistan linalodhibitiwa na Wataleban la Kashmir.

Salla alikamatwa baada ya ndege kutua kwa dharura katika jimbo la Ahmedabad, yapata maili 483 kutoka Mumbai.

Wakati huo, alikuwa ana uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa na mfanyakazi wa kampuni ya ndege mjini Delhi.

Salla aliripotiwa kuwa alimuomba mpenzi wake ahamie Mumbai lakini alikataa, na kwa kuichafulia sifa kampuni ya ndege , alitumai angepoteza kazi na kulazimika kuishi nae.

Mchunguzi wa tukio hilo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba japo Salla hakufanya utekaji wowote , kitendo alichokifanya cha kuweka waraka wenye vitisho bado kinamtia hatiani kwa kosa kujaribu kuiteka ndege kwa mujibu wa sheria ya India.

Marubani wa ndege hiyo watapokea kila mmoja Rupia 100,000 kutoka kwenye fidia atakayoitoa kwa “mkanganyiko walioupata ,” aliamuru jaji. Kila mhudumu wa ndege pia atapokea Rupia 50,000 r , na kila msafiri atalipwa Rupia 25,000.

Wakili wa Salla , Rohit Verma, alisema kuwa atakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama.

Jet Airways, ambayo wakati mmoja ilikuwa ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini India, iliahirisha safari zake zote za ndani ya nchi na za kimataifa mapema mwaka huu baada ya kupata matatizo ya kifedha.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents