Habari

Rais Mugabe apewa masaa kujiuzulu urais Zimbabwe, Nguvu yatangazwa kutumika endapo atakaidi

Baada ya kuvuliwa nafasi ya kiongozi wa juu wa Chama cha Zanu- PF Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amepewa masaa tu na Chama hicho kujiuzulu mwenyewe kwenye nafasi ya Urais wa nchi hiyo bila kutumia nguvu.

Chama tawala nchini humo leo baada ya kutangaza kuwa kimemvua uongozi Rais huyo mkongwe zaidi barani Afrika, Robert Mugabe, kimemwambia hadi kesho saa 6 mchana awe tayari ametangaza kujiuzulu nafasi ya Urais huku kikimuonya kuwa endapo atakaidi nguvu ya ziada itatumika kumng’oa madarakani.

“Rais wetu wa zamani, Robert Mugabe amepewa muda hadi kesho jumatatu saa 6 mchana awe ameshatangaza kujiuzulu nafasi ya Urais wa Zimbabwe la sivyo nguvu itatumika kumng’oa madarakani.”Imeeleza taarifa kutoka kwenye chama cha Zanu-PF iliyochapishwa kwenye ukurasa wao rasmi wa Twitter.

Soma na hii – Rais Mugabe na mkewe wakalia ‘kuti kavu’ Zanu-PF

Nafasi ya Rais Mugabe itachukuliwa na kiongozi mkuu wa Chama tawala cha Zanu PF aliyechaguliwa leo kwenye kamati kuu ya chama hicho, Emmerson Dambudzo Mnangagwa ambaye pia alishawahi kuwa Makamu wa Rais wa Mugabe kabla ya kutimuliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents