Rais Trump na Kim Jong-Un wapatana kwa masharti baada ya kukutana uso kwa uso Singapore (+video)

Hatimaye ule mkutano wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un umemalizika salama mapema leo asubuhi nchini Singapore ambapo wawili hao wamesaini nyaraka za makubaliano makubwa manne ikiwemo la kukomesha uzalishaji wa silaha za Nyuklia.

Kim Jong-Un na Rais Trump

Rais Trump akizungumza mbele ya mamia ya waandishi wa Habari, amesema leo viongozi hao wawili wamesaini mambo mawili makubwa ya kimahusiano ya kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili na kitendo hicho kimerudisha uhusiano mwema baina ya mataifa hayo yenye nguvu zaidi kijeshi duniani.

Trump na Kim walikaa kikao cha watu wawili kwa masaa mawili kabla ya kukutana na waandishi wa habari na kusaini makubaliano hayo.

Kwa mujibu wa maelezo ya mtandao wa shirika la Utangazaji la AFP, makubaliano hayo manne ni kuanzisha uhusiano mpya baina ya mataifa hayo, kudumisha amani ya kudumu katika rasi ya Korea na maafikiano ya Panmunjom ya Aprili 27, 2018 ya Korea Kaskazini kuhakikisha inaangamiza kabisa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.

Hata hivyo, Trump amesema kuwa kuna masharti wawili hao wamepeana na kama Kim Jong-Un atayashindwa au atataka mabadiliko basi watawasiliana kwa simu.

Tazama mkutano huo hapa chini wababe hao wakisaini nyaraka za makubaliano na kutoa hotuba fupi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW