Habari

Rais wa Ufilipino amkashfu Mungu ‘mpumbavu, alitegemea nini kuwaumba Adam na Eva’

Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte ameibua mjadala mzito kwa wakristu nchini humo baada ya kutoa kauli ya kumuita Mwenyezi Mungu ‘Mpumbavu’ kwa kitendo cha kumuumba Eva na kumuweka na Adam katika bustani ya Edeni huku akiwakataza wasile tunda la katikati huku akijua kitu hicho hakiwezekani.

Rodrigo Duterte

Duterte ametoa kauli hiyo Ijumaa Juni 22, 2018 kwenye mkutano wa Kitaifa wa Teknolojia unaofanyika kila mwaka  Jijini Davao.

Akipinga historia ya Adam na Eva iliyoandikwa kwenye Biblia huku akilipinga Kanisa Katoliki nchini humo, Duterte amesema kuwa alichokiona kwenye kitabu hicho ni upuuzi mtupu kwani anaamini Mungu hawezi mwenyewe halafu akaharibu mwenyewe.

Sijui hili ni dhehebu gani mnaliita Katoliki, kila siku linalalamika Duterte.. Duterte.. nadhani mnaabudu Mungu Mwingine yule Mpumbavu mnayesema alimuumba Adam halafu akamuumba Eva kisha wakaa sehemu moja halafu Mungu huyo huyo akawakataza wasifanye mapenzi kwani ni dhambi, hivi unadhani alitegemea nini kuwaweka pamoja kwenye bustani ya Edeni?,“amesema Duterte kwa kuwauliza maelfu ya watu waliohudhuria kwenye mkutano huo na kufunguka zaidi.

Yaani aumbe mwenyewe halafu abomoe mwenyewe huyo Mungu ni mpumbavu, sisi wote tunaamini tumekuja duniani kuzaliana na hata Mungu aliagiza hivyo.“amesema Duterte na kulionya Kanisa Katoliki nchini humo linalotangaza kuwa anakiuka haki za binadamu na maandiko ya Mungu kwa kitendo cha kuruhusu Polisi kuwauwa watu wanaotumia madawa ya kulevya nchini humo.

Mungu ninayemjua mimi hafanani na binadamu hata kidogo kwa sababu kuna binadamu wengine wana mambo ya kishetani na hawastahili kuishi duniani, mimi mwenyewe nasoma Biblia hao Wakatoliki wanaomfananisha Mungu ninaye mjua mimi na huyo wa kwao Mungu Mpuuzi siwaelewi? na hata kama wakisema sina hofu na Mungu kwani inawauma nini?“amesema Duterte.

Kauli ya Duterte sio ya kwanza kuliponda Kanisa Katoliki nchini humo kwani mwezi uliopita akihutubia jamii ya Wafilipino waishio Korea Kusini alinukuriwa akilipiga vita Kanisa Katoliki nchini mwake.

Mwezi Aprili pia wakati akihutubia taifa hilo kubwa lenye watu milioni 103, Duterte alisema kuwa Mungu anayemuamini yeye ni wa kipekee tofauti na Makanisa ya Mbwa Mwitu (akililenga Kanisa Katoliki) yanayopotosha umma.

Rais Duterte ni Mkisto na ni muumini wa Kanisa Katoliki ila ameacha kuhudhuria kwenye misa tangu mwaka 2016 baada ya kutangaza kuwa kama angelikuwa anawasikiliza Mapadri basi asingeliweza kufikia malengo yake alipokuwa Meya wa Jiji la Davao na mpaka sasa anaamini kuwa kuna Allah ila sio Mungu anayeabudiwa na waumini wa Kanisa Katoliki.

Tayari Makamu wa Rais wa Ufilipino, Leni Robredo na maafisa mawasiliano Ikulu wamekutana na viongozi wa Kanisa Katoliki kwa mazungumzo juu ya matamshi ya Rais Duterte.

Tazama kipande kifupi cha hotuba ya Rais Duterte akimtukama Mwenyezi Mungu kwenye na kulishambulia Kanisa Katoliki.

https://youtu.be/-udzuiKadB4

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents