Burudani

Rama Dee atoa sababu za kuachia video nyingine badala ya ‘Nibebe’

Mkali wa RnB Bongo, Rama Dee ameamua kutoa ufafanuzi wa kutoa achia video ya ngoma yake mpya ya ‘Nibebe’ aliyokuwa akifanyia media Tour.

Akiongea na Bongo5, Rama Dee ameeleza kuwa video ya ‘Nibebe’ ipo ila ameamua kuachia ‘Kwa akili Yangu’ ni moja ya utaratibu wake kama mwanamuziki katika game.

“Kila mwanamuziki anakuwa na utaratibu wake katika utoaji wimbo, utaratibu wa Rama Dee ni kama hivyo, nimeamua kutoa video ya wimbo mwingine then nitaendelea na ratiba nyingine ya Nibebe,” amesema msanii huyo.

Pia akaongeza kuwa “Video ya Nibebe tayari nimesha-shoot, tunachosubiri ni kumaliza baadhi ya vitu vitu ili iweze kukaa juu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents