Habari

Rayvanny atoa wito kwa wasanii ‘kidogo tunachopata, tusaidie ndugu zetu wenye Magonjwa’

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka WCB, Rayvanny amewataka Watanzania wenye uwezo kwajitoe japo kidogo kuwasaidia wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali Hospitalini.

Rayvanny

Rayvanny amesema hayo, baada ya jana kutembelea katika Hospitali ya Muhimbili kumjulia hali mama  aliyekuwa anasumbuliwa na jicho kutoka Mbeya, ambaye wiki iliyopita video zake zilisambaa mtandaoni zikimuonesha akiomba msaada wa matibabu.

Nashukuru Mungu Leo Nimepata Nafasi Kutembelea Hospitali Ya Muhimbili, Kumuangalia Yule Mama mwenye tatizo la jicho. Kwangu Leo imekua kama darasa na Sehemu Ya kujifunza, kutokana na Hali Ya ndugu zetu pale Hospitali.Nilienda Kwa Ajili Ya Yule Mama lakini nikajikuta naenda Kwa Wodi Nzima…. KIDOGO NILICHOKUA NACHO NIKASAIDIA WODI NZIMA…. Maana Ya Mimi kupost Sio kujikweza Ila nikukumbushana Kwa Kidogo Tunachokua nacho Tusiache kusaidia ndugu zetu wenye Magonjwa,Matatizo mbalimbali na Wasiojiweza…. MUNGU AWABARIKI

Rayvanny ndiye aliyeanza kutoa taarifa za mama huyo aliyekuwa anasumbuliwa na jicho na tayari ameshapatiwa matibabu siku ya jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents