Habari

RC Gambo atoa onyo kwa watakaoandamana Arusha ‘Upanga haujaribiwi shingoni’

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ametoa onyo kali kwa watu watakaothubutu kuandamana mkoani humo baada ya kuzagaa kwa taarifa mitandaoni kuwa tarehe 26 April kutakuwa na maandamano ya nchi nzima.

Tokeo la picha la Mrisho gambo
Mrisho Gambo

RC Gambo amesema Arusha ni mji wa kitalii hivyo asingependa kuona usalama na amani inatoweka mkoani humo na kupoteza watalii ambao wanasaidia kukuza uchumi wa nchi.

Arusha ni mkoa wa kitalii hatuwezi kuruhusu mambo yatakayoharibu uchumi na usalama wetu, kama kuna kikundi chochote kinampango kutujaribu, tunatoa tahadhari na kuwakumbusha kuwa upanga haujaribiwi shingoni,“ameeleza Mrisho Gambo kwenye taarifa yake.

Onyo la Gambo ni muendelezo wa maonyo mengine yaliyotolewa na viongozi wengine serikalini akiwemo Rais Magufuli juu ya watu watakaoandamana siku hiyo.

Soma zaidi – Rais Magufuli atoa onyo kali kwa watu wanaopanga kuandamana

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents