Tupo Nawe

RC Makonda amuomba radhi Rais Magufuli kisa nusu bei ‘nakuahidi sitorudia hiki kitendo’

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda amemuomba radhi Rais Magufuli kwa kauli yake ya vinywaji kuuzwa nusu bei.

Akiongea mbele ya Rais Magufuli Ikulu leo Machi 25, 2019, RC Makonda amesema kuwa anaomba radhi kwa kuagiza vinywaji vyote viuzwe nusu bei jijini Dar Es Salaam, endapo Taifa Stars ikifuzu.

“Rais naomba radhi kwa tukio la jana, watu wamelewa sana na nina uhakika kuna uwezekano watu hawajafika Maofisini, nitumie fursa hii kuomba radhi Maboss wote ndani ya Dar Es Salaam. Hali ilikuwa sio hali nakuahidi Rais sitorudia hiki kitendo cha nusu bei,” RC Makonda.

Wiki iliyopita RC Makonda aliagiza kuwa endapo Taifa Stars itawafunga Uganda na kufuzu AFCON, basi vinywaji vyote Jijini Dar Es Salaam vitauzwa nusu bei.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW