DStv Inogilee!

RC Makonda kuwashughulikia wanaowadhalilisha wahudumu wa baa na wafanyakazi wa nyumbani

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amepanga kukutana na makundi ya watu mbalimbali ikiwemo wahudumu wa Bar, Hotel, wafanyakazi wa Saloon na wafanyakazi wa nyumbani kwa lengo la kusikiliza kero na malalamiko yao baada ya kubaini wengi wao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji ikiwemo kutolewa lugha za matusi kutoka kwa baadhi ya wanaume wasiojiheshimu.

RC Makonda amesema kuwa katika mkutano wake na makundi hayo atataka kufahamu masuala ya mishahara, ajira,changamoto wanazopitia na suala zima la usalama wanaporudi majumbani usiku wa manane ambpo ameeleza kuwa anachokitaka ni kuona kila mtu anaheshimu kazi ya mwenzake.

Hayo yote yamejiri leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya wanawake yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW