Burudani

Redsan amshushia kichapo Producer wake Sappy, aahidi kumkamata Promota aliyemtapeli Tiwa Savage

Msanii wa muziki nchini Kenya, Redsan usiku wa kuamkia leo amemshambulia mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania ambaye anafanyia kazi zake Jijini Nairobi, Dkt. Sappy .

Kwa mujibu wa sauti iliyovuja mtandaoni, inasikika Redsan akimfokea Sappy na kumpiga makofi huku akihoji kwa nini hakupokea simu zake.

Kwa mujibu wa Sappy amesema kuwa walikuwa studio na msanii wa muziki, Avid ghafla Redsan aliingia akidai kuwa kwanini Sappy hapokei simu yake na kwa nini hakutokea kwenye uzinduzi wa album yake iliyozinduliwa wikiendi iliyopita.

Baada ya kauli hiyo, Redsan alianza kurusha ngumi na kuanza kusukumana na kuanza kurushiana maneno machafu.

Kwa upande mwingine, Redsan ameahidi  kumtafuta promota aliyemuingiza kwenye mataa msanii wa muziki kutoka Nigeria, Tiwa Savage.

Tiwa Savage alikuwa ni moja ya wasanii wakubwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa album ya Redsan, Soma zaidi – Msanii kutoka Nigeria Tiwa Savage aachwa solemba na Promota aliyempeleka Kenya .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents