Burudani

Rihanna ampeleka baba yake mzazi mahakamani kisa jina la familia

Mwanamuziki kutoka Marekani Robyn Rihanna Fenty alimaarufu Rihanna amshtaki Baba yake Mzazi (Ronald), kwa kosa la kutumia chapa ya familia “Fenty” kinyume cha sheria kwa lengo la kujiingizia kipato kwa kufungua kampuni yake “Fenty Entertainment”. Mtandao mmoja nchini Marekani umeripoti kuwa mwimbaji “Rihanna Fenty” amempeleka Baba yake Mahakamani akidai anatumia umaarufu wake kutengeneza kipato akiwa na mfanyabiashara mwenza, Moses Perkins.

Mzee Fenty amekuwa akifanya kazi kama wakala wa Riri kinyume cha sheria, na tayari amepata show ya dola million 15 ambayo ni ziara pamoja na matamasha mawili huko Latin America. Show nyingine ni za Staples Center mjini Los Angeles, T-Mobile Arena mjini Las Vegas zote mbili akivuta mkwanja wa dola 400,000

Rihanna ameenda mbali zaidi na kutaka fidia toka kwa mshua wake, pia ameitaka Mahakama kusimamisha shughuli za kampuni hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2017, pamoja na yote hayo Rihanna ametangaza kuja na accessories zake ambazo zitaingia sokoni hivi karibuni.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents