Shinda na SIM Account

RIPOTI: Meli yenye bendera ya Tanzania yakamatwa na vilipuzi nchini Ugiriki

Jeshi la Majini nchini Ugiriki limeishikilia meli yenye bendera ya Tanzania ambayo  imebeba vilipuzi ikielekea nchini Libya.

Meli hiyo inadaiwa kusafirisha vilipuzi hivyo kutoka Uturuki kwenda Libya kinyume na marufuku iliyowekwa ya kutosafirisha silaha kwenda Libya.

Kwa mujibu wa Mtandao wa BBC Maafisa wanasema meli hiyo ilikuwa imebeba kreti 29 zilizojaa vilipuzi pamoja na kemikali zinazotumiwa kuunda vilipuzi.

Wizara ya Usafiri wa Majini nchini humo kupitia shirika la habari la Ugiriki la ANA imesema meli hiyo ilisimamishwa ikiwa katika kisiwa cha Crete kusini mwa Ugiriki wikiendi iliyopita baada ya kutiliwa shaka na Jeshi la Usalama la Majini.

Chanzo:BBC

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW