Habari

RIPOTI: UDSM yadahili wanafunzi wengi kuliko uwezo wake, Ubora wa elimu wahofiwa kushuka

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimebainika kudahili wanafunzi kwa zaidi ya mara tano ya uwezo wake na kuibua hofu ya kushuka kwa ubora wa elimu unaotolewa kwa wahitimu wake.

Changamoto hiyo imeibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad, katika ripoti yake ya ukaguzi wa mwaka wa fedha 2017/18, iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma Jumatano.

Katika ripoti yake kuhusu ukaguzi wa mashirika ya umma, CAG Assad anabainisha kuwa mnamo mwaka 2016/17, UDSM ilidahili wanafunzi kwa zaidi ya asilimia 560 ikilinganishwa na mpango wake.

Hii ina maana kuwa idadi ya wanafunzi waliodahiliwa ilipita uwezo wa chuo hicho. Zaidi ya hayo, nilibaini kuwa udahili haukuwa umetolewa taarifa kwa kiwango ambacho kila kitivo kilielewa idadi ya wanafunzi waliotakiwa kudahiliwa,“amebainisha.

Majadiliano na baadhi ya maofisa yalionyesha kuwa kiwango cha juu cha udahili huo hakikuwa na uwiano na rasilimali nyingine za chuo kama vile rasilimali watu na miundombinu ili kukidhi bila shida ongezeko hilo.

CAG Assad amebainisha kuwa ongezeko hilo kubwa la udahili linahatarisha ubora wa elimu watakaopata wahitimu, hivyo kuwa na athari ya muda mrefu kwa maendeleo ya taifa.

Ninapendekeza UDSM itayarishe na kutekeleza mpango wa udahili ambao utatokana na tathmini ya mahitaji na uwezo wa chuo kikuu,” amesema Prof. Assad .

Chanzo: Nipashe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents