Habari

Ronaldo hakamatiki kwa Hat-trick, Aiweka nafasi nzuri Ureno kufuzu EURO 2020

Mshambuliaji wa klabu ya Juventus na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo usiku wa kuamkia leo ameisaidia timu yake ya Taifa kuibuka na ushindi wa goli 6-0 dhidi ya Lithuania, Huku Ronaldo akipiga Hat-trick ya 55 katika maisha yake ya soka.

Ushindi huo wa jana umeifanya Ureno kushika nafasi ya pili katika kundi B ikiwa nyuma ya Ukraine ambayo tayari imeshafuzu.

Kwa sasa Ureno itahitaji ushindi kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Luxembourg, Ambapo endapo Ureno itafungwa au kutoa sare yoyote ile na Serbia ikashinda mchezo wake wa mwisho basi Ureno itakuwa imetolewa kushiriki michuano ya EURO 2019.

Mpaka jana mataifa 10 tayari yameshafuzu, Belgium, Italy, Poland, Russia, Spain, Ukraine, Turkey, France, England na Czech Republic.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents