Burudani

Sakata la R.Kelly la unyanyasaji mabinti kingono laibuka upya, wanawake wengine wawili wajitokeza wakiwa na ushahidi

Wanawake wengine wawili wamejitokeza na madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanamuziki wa R&B,R Kelly. Rochelle Washington na Latresa Scaff walizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuwa walipewa kinywaji pamoja na madawa ya kulevya mara baada ya tamasha la mwanamuziki huyo lililofanyika Baltimore miaka ya 1990.

Kwa mujibu wa BBC. Wanawake hao walisema kuwa mwanamuziki huyo aliwapeleka katika chumba cha hoteli bila ridhaa yao na kutaka kufanya nao mapenzi.

Kelly mwenye umri wa miaka 52, amekuwa akishutumiwa kwa madai ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake kwa miongo kadhaa lakini hakuwahi kukamatwa wala kukiri makosa yake.

akizungumza na waandishi wa habari , wanasema kuwa wakati huo ambao Kelly aliwachukua kwenda kwenye tamasha walikuwa vijana wadogo.Vilevile walishindwa kusema ni mwaka gani sahihi ambao walinyanyaswa kingono bali walisema ni kati ya mwaka 1995 au 1996.

Bi Scaff mwenye umri wa miaka 40, anasema kuwa katika sherehe hiyo ya muziki walipewa madawa ya kulevya aina ya ‘cocaine’, bangi na pombe na kualikwa kumsubiri mwanamuziki katika chumba cha hoteli.

Wakiwa katika chumba hicho, waliambiwa wavue nguo kwa sababu Kelly alikuwa karibu anafika

Mwanamuziki huyo alifika akiwa ameacha sehemu yake ya siri wazi, Bi.Scaff aliwaalika ili wafanye mapenzi wakiwa watatu kwa pamoja.

Bi Washington, ambaye sasa ana umri wa miaka 39 alikataa na kwenda bafuni wakati ambapo Scaff alibaki na kufanya naye mapenzi ingawa sio kwa ridhaa yake , ni kwa sababu ya kulewa pombe na madawa ya kulevya, alisimulia.

Bi.Scaff alisema kuwa ameamua kuliweka jambo hilo wazi kwa sababu wao ni waathirika kama waathirika wengine wa ngono.

Wanawake hao wawili waliwakilishwa na wakili mashuhuri Gloria Allred na vilevile aliwakilisha wanawake wengine ambao walitoa malalamiko yao dhidi ya Kelly.

Akituma ujumbe kwa mwanamuziki huyo maarufu duniani alisema: ” Huna pa kukimbilia au kujificha. Umeweza kukana makosa yako maovu kwa muda mrefu.”

R Kelly ambaye jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly, amekutana na shutuma za unyanyasaji wa kingono kwa miaka zaidi ya ishirini.

Katika makala ya hivi karibuni inayoitwa , ‘Surviving R Kelly’, ambayo ilikuwa inaoneshwa katika chaneli moja ya televisheni inayoitwa lifetime, imeeleza namna ambavyo amefafanua madai yake dhidi ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake. Hata hivyo wakili wa Kelly amesitisha makala hiyo isiendelee kutumika.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents