Burudani ya Michezo Live

Sanamu ya Mwl. Nyerere aliyokabidhiwa Rais Magufuli na Waziri Kigwangalla yazua gumzo mtandaoni, Wengine waifananisha na Steve Nyerere

Jana Julai 9, 2019 kulikuwa na hafla ya uzinduzi wa Hifadhi mpya ya wanyamapori ya Burigi-Chato, Hafla ambayo ilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla mara baada ya kumkabidhi Sanamu hiyo ya Baba wa Taifa. Rais Dkt. Magufuli ametoa maelekezo kuwa Sanamu hiyo aliyokabidhiwa ijengewe eneo zuri katika hifadhi hiyo ya Burigi Chato ili watalii wakija waweze kumjua zaidi Muasisi wa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwenye uzinduzi huo, Rais Magufuli alikabidhiwa sanamu ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla yenye ujumbe maalum kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira ya wanyama pori.

Muonekano wa sanamu hiyo, umezua mijadala tofauti tofauti kwenye mitandao ya kijamii wengi wakionekana kushangazwa na muonekano wake wakidai kuwa hauendani hata kidogo na sura ya Mwalimu Nyerere.

MAONI YA WADAU KUTOKA TWITTER.

https://twitter.com/Apollomargwe/status/1148832242870968320

https://twitter.com/SheriiiMalia/status/1148864636076400641

KUTOKA INSTAGRAM

dennis_louis_

mbona hii sanamu inafanana na Mzee malekela baba yake lemutuz?

seviour_son

Jamaaaaan amkeeeen Kuna Nyerere Mpya Huku 🌚🌚🌚😀😀…
Huyu Ndugu Yake labda😂

mwanakhamis_masoud

Hy ni sanamu ya nani?????

itambikojunior

Ila huyo itakuwa mwalimu wa maarifa ila siyo sanamu ya mwalimu Nyerere

k_wa_tatu

@hamisi_kigwangalla mkuu,
Huyo sio nyerere tunayemfahamu….
Ni vyema ukaibadili

iamkenny255

Mmmh! Huyo mbona kama Steve nyerere au macho yenu yanaona kama Mimi?

jm.shenyagwa

Naomba tuelewane, Hii ni sura ya baba wa Taifa kwa sasa hivi, siyo ya kipindi cha uhai wake. Mwisho wa mjadala🔥🔥😂

Je, unadhani kweli sanamu hiyo imekosewa au ni macho ya watu hao wameshindwa utambuzi wa sura ya baba wa Taifa?

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW