Burudani

Sauti Sol waungana na maelfu ya Wakenya kupinga unyanyaswaji wa MaDJ’s

Kundi la muziki kutoka nchini Kenya, Sauti Sol limeungana na maelfu ya Wakenya mtandaoni kupinga hatua ya serikali ya jiji la Nairobi kuwakamata MaDeej’s wanaopiga muziki kuanzia saa sita usiku kwa madai kuwa wanachafua mazingira kwa makelele.

Sauti Sol

Sauti Sol wamesema kuwa huwezi kukamilisha muziki katika klabu kama hakutakuwa na DJ, Hakuna mtu mwingine atakayefanya sherehe yako inoge kama hautakuwa na Dj na kutamka rasmi kuwa wanaungana na Wakenya wenzao katika kutafuta haki juu ya ukamatwaji wa MaDJ’s ambao wanajitafutia riziki kupitia mikono yao.

As an artist, who do you turn to for support when you have new content out? As a fan, who do you go to when you’re at a party, event or in the club and want to request for your fav joint? The Dj! Therefore, let’s all join the thread and show support for our DJs.“wameandika Sauti Sol kupitia ukurasa wao wa Twitter.

Maelfu ya Wakenya jana na leo wameanzisha mtandaoni Hashtag maalumu ya #StopArrestingDJs kuishinikiza serikali na Gavana wa Jiji la Nairobi, Miko Sonko kuwaachia maDJs wote waliokamatwa kuanzia wikiendi iliyopita.

Kikosi hicho kinachowakamata MaDJs kinaongozwa na Jeshi la Polisi kushirikiana na watu wa Mamlaka ya Mazingira nchini Kenya (NEMA) na mpaka leo asubuhi Madeej’s wawili Riggz na Tremor pekee ndio walioachiwa kwa dhamana huku wengine wakiwa bado wameshikiliwa.

Hata hivyo, Jana DJ maarufu nchini Kenya Creme del a creme alienda hadi Kituo Kikubwa cha Polisi jijini Nairobi na kufanikiwa kuwatoa Madeej’s wawili walioshikwa kutoka  Alchemist club.

Watu wengi nchini Kenya wamelaumu hatua hivyo wakidai kuwa ni unyanyasi huku wakitaka hatua hiyo ianzie kwa wamiliki wa Club na kumbi za starehe na sio kuwakamata moja kwa moja Madeej’s.

Wasanii na watu maarufu nchini Kenya wameshaunga mkono kampeni hiyo mitandaoni kushinikiza Madeej’s wasikamatwe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents