Aisee DSTV!
SwahiliFix

Serikali yamjibu Zitto Kabwe kuhusu onyo kwa magazeti yaliyoandika uchambuzi wa ripoti ya CAG uliofanywa na ACT Wazalendo

Baada ya kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kudai kuwa serikali imetoa onyo kali kwa magazeti yaliyoandika uchambuzi wa ripoti ya CAG uliyofanywa na chama hicho, hatimaye serikali imemjibu kwa kumwambia aache kuingilia masuala ya kiutendaji.

Dkt. Hassan Abbas na Zitto Kabwe

Majibu hayo yametolewa na Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kumwambia Kiongozi huyo kuwa “Kama hili ni andiko lako pokea/puuzia ushauri: 1.Usilete siasa ktk taaluma ambayo bahati mbaya huijui misingi yake.Walioandikiwa wamejua/kukiri kosa lao. 2.Kama waliandikiwa, wakaripoti kwako sasa tumejua wewe ndie Mhariri Mkuu unaewapotosha kila siku, Acha.“.

Zitto Kabwe awali ali-tweet kutoa taarifa hiyo ya Serikali kuwa imetoa onyo kwa magazeti ambayo hakuyataja kwa majina.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW